LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKAMBA AWAUMBUA WANAOTUMIA KIGEZO CHA GESI KUOMBA RIDHAA YA URAIS.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknologia January Makamba akitangaza jana nia ya kugombea Urais (CCM) katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Na: ELISA ANATORY   0763345064
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknologia January Makamba ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Akitangaza nia hiyo jana Jijini Dar es salaam, Makamba alisema kuwa ili Tanzania iweze kupiga hatua kimaendeleo, ni lazima iwe na kiongozi shupavu, mwaminifu, mwenye busara, mwenye ujuzi na uzoefu katika kuliongoza Taifa.

Makamba alitaja baadhi ya vitu ambavyo atavipa kipau mbele pale atakapopewa na fasi hiyo kuwa ni pamoja na kutokomeza ufisadi, rushwa, kupambana na umaskini pamoja na maadili kwa viongozi hapa nchini.

Aidha aliongeza kuwa atahakikisha anafufua viwanda vilivyokufa kutokana na ukosa mali ghafi, kutoa mikopo ya kutosha kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu ili uongeza kiwango cha elimu, ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha elimu kote nchini ikilinganishwa na ilivyo sasa.


Kuhusu mapato ya gesi Makamba aliwataka watanzania kuachana na baadhi ya wagombea wanaosema kuwa watakapoingia madarakani katika kipindi cha miaka mitano nchi itanufaika na nishati ya gesi ambapo alibainisha kuwa nishati hiyo itaanza kulinufaisha taifa baada ya miaka kumi ijayo.
Makada wa CCM na Wananchi wakimsikiliza January Makamba katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam jana.

No comments:

Powered by Blogger.