LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA NYUMBA 13 JIJINI MWANZA HATARINI. HALMASHAURI YASUBIRI MAAFA YATOKEE KWANZA.

Miongoni mwa Mawe yaliyo katika Kilima cha Mtaa wa Nyerere B, Kata Mpya ya Mabatini Jijini Mwanza
Na:George GB Pazzo 
Zaidi ya nyumba Kumi na Tatu (13) zilizopo katika Mtaa wa Nyerere B, Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, ziko hatarini baada ya nyumba hizo kujengwa chini ya eneo lenye mwinuko wenye jiwe kubwa ambalo liko hatarini kuporomoka.

Wakizungumza jana katika Kampeni ya Kata kwa Kata, Mtaa kwa Mtaa ya Rado Metro Fm, baadhi ya Wakazi wanaoishi katika Mtaa huo walisema kuwa maisha yao yako hatarini kutokana na jiwe hilo kuonyesha dalili za kuporomoka.

Walisema kuwa wanalazimika kuendelea kuishi katika nyumba hizo kukosa eneo mbadala kuhamishia makazi yao ambapo waliiomba Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupasua jiwe hilo ili kuwanusuru na hatari iliyopo.

Kwa pamoja, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Nyerere B, Themistoclass Mtenga na Katibu wake Ommary Mussa Msalika walitoa rai kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kulishughulikia haraka suala hilo, ambapo walibainisha kuwa uongozi huo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza uliahidi kulishughulikia tangu mwezi disemba mwaka jana lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote ambazo zimezochukuliwa.

"Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza tulimfuata na kumweleza juu ya jiwe hili na yeye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza walikuja wakaliona, lakini mpaka sasa hatujui kinachoendelea na hata tukifuatilia tunaambiwa hakuna pesa za kupasua jiwe hilo". Walisema viongozi hao huku wakiongeza kuwa;

"Tulipohitaji pesa za mfuko wa dharura kutoka halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kupasua jiwe hilo, tulielezwa kwamba fedha hizo haziwezi kutolewa maana dharura yenyewe bado haijatokea hali inayoashiria ukweli kwamba uongozi wa jiji la Mwanza unasubiri jiwe hilo lilete maafa kwanza ndipo fedha za maafa ziweze kutolewa".

Mwishoni mwa mwaka jana katika Mtaa Eso eneo la Sinai ndani ya Kata hiyo ya Mabatini, jiwe kama hilo liliporomoka na kusababisha madhara kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kwa watu watatu wa familia moja waliokuwa wamelala usiku wakati linaporomoka.
Hili ni jiwe ambalo limemeguka na nusra liporomoke na kuangukia nyumba za wananchi wanaoishi katika Mtaa wa Nyerere B, Kata Mpya ya Mabatini Jijini Mwanza.
Mmoja wa Wakazi wa Mtaa wa Nyerere B, Mabatini (kulia) akielezea hatari ya mawe iliyopo katika Mtaa wake.
Mmoja wa Wakazi wa Mtaa wa Nyerere B, Mabatini (kushoto) akielezea hatari ya mawe iliyopo katika Mtaa wake.
Mmoja wa Wakazi wa Mtaa wa Nyerere B, Mabatini (Kulia) akielezea hatari ya mawe iliyopo katika Mtaa wake.
Mmoja wa Wakazi wa Mtaa wa Nyerere B, Mabatini (kushoto) akielezea hatari ya mawe iliyopo katika Mtaa wake.
Katibu wake Ommary Mussa Msalika ambae ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Nyerere B, Kata ya Mabatini Jijini Mwanza na Katibu wa Mwenyekiti wa Mtaa huo.
 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Nyerere B, Themistoclass Mtenga (Kushoto) akizungumza na GB Pazzo (Kulia).
Hii ni Moja ya Nyumba ambayo iko katika hatari ya Kuporomokewa na Jiwe lililopo katika Kilima cha Mtaa wa Nyerere B, Kata Mpya ya Mabatini Jijini Mwanza ambapo wenyeji wa nyumba hii wameikimbia hii nyumba ili kuyanueuru maisha yao.
Huu ni Mtaa wa Nyerere B, Kata Mpya ya Mabatini Jijini Mwanza ambapo Mtaa huu upo eneo la Mwinuko (Kilima) huku kukiwa na ujenzi holela katika maeneo yenye mawe ambayo yanahatarisha Maisha ya Wakazi wa Mtaa huu wanaoishi katika nyumba zaidi ya 13.
Credit:Kata kwa Kata, Mtaa kwa Mtaa ya Radio Metro Fm

No comments:

Powered by Blogger.