LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKEREKA NA TABIA YA KUTUPA VICHANGA KATIKA DAMPO LA MABATINI SOKONI JIJINI MWANZA.

GB Pazzo (kushoto) kutoka Radio Metro akizungumza na Rose Magabe ambae ni mmoja wa wafanyabiashara wa Soko Mjinga Mabatini Jijini Mwanza.
Ni katika dampo la Soko hilo maaruku kama Soko Mjinga ambalo mbali na kukithiri uchafu, limeingia katika hatari nyingine ambapo inaelezwa kuwa mara kwa mara vichanga (watoto wachanga) vimekuwa vikitupwa katika dampo hilo.
Picha na Rogger William
Wakizungumza na Radio Metro jana, baadhi ya wakazi wa Mabatini pamoja na wafanyabiashara wa Soko la Mabatini/ Soko Mjinga walieleza kukereka na tabia hiyo ambapo walitoa rai kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha kuwa Uchafu katika dampo hilo unaondolewa mara kwa mara tofauti na hivi sasa ambapo uchafu huondolewa mara moja kwa zaidi ya miezi miwili ili kuondoa uwezekano wa baadhi ya watu wenye huruka mbaya ya kutupa vichanga katika dampo hilo.
GB Pazzo akiwa katika Mahojiano na Rose James Mwita ambae ni Mfanyabiashara katika Soko la Mabatini Jijini Mwanza.
Elizabeth Chacha (Kushoto) ambae ni Mmoja wa Wafanyabiashara wa Soko Mjinga Mabatini (Kushoto) akizungumza na GB Pazzo.
Credit: Kata kwa Kata, Mtaa kwa Mtaa II ya Radio Metro Fm

No comments:

Powered by Blogger.