LIVE STREAM ADS

Header Ads

MACHINGA UNITED YA JIJINI MWANZA YAPOKEA MSAADA WA JEZI KUTOKA KWA OYUGI.

Ayubu Michael Oyugi (Wa kwanza Kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Pamba Jijini Mwanza akiikabidhi msaada wa Jezi Timu ya Soka ya Machinga United
Na:George GB Pazzo
Timu ya Soka ya Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza ya Machinga United, imepokea msaada wa jezi jozi moja zenye thamani ya shilingi Lakini mbili na elfu hamsini ambapo Msaada huo umelenga kuiimarisha zaidi timu hiyo.

Msaada huo ulitolewa jana na Ayubu Michael Oyugi ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Pamba Jijini Mwanza, ambae ameelezea kufurahishwa kwake na uanzishwaji wa timu hiyo.

Alisema binafsi ameguswa na uanzishwaji wa Timu hiyo ya Machinga United kwa kuwa anaamini ya kwamba Michezo ni ajira hivyo matumaini yake ni kuona timu hiyo ikizalisha ajira kwa vijana kupitia Michezo.

Hidaya Juma (Concod) ambae ni Katibu wa Mchinga United pamoja na Dickson Peter ambae ni Kaptain wa timu hiyo ambayo inashiriki Michuano ya Ligi ya Ng’ombe Jijini Mwanza kwa timu zilizo daraja la nne ambayo inaendelea katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Buhongwa, walitoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kwa wingi ili kuisaidia kwa lengo la kuiwezesha kusonga mbele kimichezo.

Walitoa pongezi kwa Mfanyabiashara MUKESHI, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslauns Mabula pamoja na Mkurugenzi wa Jiji hilo Halifa Hida kwa namna ambavyo wamekuwa wakijitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha kwamba Machinga United inasimama ili iweze kupanda daraja.
Timu ya Machinga United inayomilikwa na Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza
Ayubu Michael Oyugi ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Pamba Jijini Mwanza.
Hidaya Juma (Concod) ambae ni Katibu wa Mchinga United 
Dickson Peter ambae ni Kaptain wa timu ya Machinga United
Picha ya Pamoja.
Credit:Radio 99.4 Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.