LIVE STREAM ADS

Header Ads

MMOJA AFARIKI DUNIA HUKU WENGINE WAKINUSURIKA BAADA YA KUBUGIA CHAKULA CHENYE SUMU.

Na:Ofisi ya RPC Mara
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ghati Itumbo  amefariki dunia katika kijiji cha Maji Moto wilaya ya Serengeti  Mkoani Mara, baada ya  kula chakula kinacho sadikiwa   kuwa na  sumu katika mgahawa mmoja uliokuwa ukiuza chakula Kijijini hapo.

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara Ernest Kimora aliyasema hayo juzi wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo aliongeza kuwa katika tukio hilo pia kuna watu watatu walinusurika kifo baada ya kula chakula hicho.

Aliwataja walionusurika kuwa ni Elizabeth Juma, Pendo Mussa pamoja na Neema Nelson ambapo wote wamelazwa katika hospitali ya DDH Mugumu ya Mkoani humo kwa ajili ya matibabu.

Alisema hakuna yeyote aliekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa jeshi la polisi Mkoani Mara linaendelea na uchunguzi wake ili kubaini waliohusika ambapo alibainisha kwamba mabaki ya chakula kilicholiwa na watu hao yamechukuliwa kwa  ajili ya uchunguzi zaidi.


Hata hivyo Kaimu Kamanda Kimora aliwaasa wananchi kuepukana na tabia ya kula  vyakula ovyo katika maeneo yasiyo rasmi hususani katika maeneo yenye mikusanyiko  wa watu ili kuepukana na athari zinazoweza kuwakumba.

No comments:

Powered by Blogger.