LIVE STREAM ADS

Header Ads

PATA MSHANGAO KATIKA VIDEO MPYA YA MR. ENGLISH-RAZZ MA TAZZ.

Msanii Mr.English kutoka Jijini Mwanza ameachia Video ya wimbo wake unaofahamika kwa jina la RAZZ MA TAZZ. Mr.English kwa pamoja ameachia Audio na Video ya wimbo huo ambao umepokelewa vyema wapenda burudani wote.

Wimbo wa Razz Ma Tazz umetengenezewa katika Studio za OVER THE CLASSIC zilizopo Jijini Mwanza. Video yake haichoshi kutazama, lakini pia hata Audio yake haichoshi ukiisikiliza. Kwa ujumla kazi ni nzuri na pengine ndiyo maana Razz Ma Tazz imepokelewa vyema.

"Razz Ma Tazz maana yake ni mshangao, kumuweka mtu au watu katika umakini fulani kwa ajili ya kusikiliza au kutazama kinachojili". Mr. English ameiambia Binagi Tv inayopatikana kupitia BINAGI MEDIA GROUP. 
Sasa itazame Razz Ma Tazz ili nawe upate Mshangao.
TAZAMA NA DOWNLOAD RAZZ MA TAZZ HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.