LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKAZI WA UNGUJA JIJINI MWANZA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MFUMO WA MAJITAKA.

Mary Dismas Elias (Kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Afya Mtaa wa Unguja Kata ya Mbugani Jijini Mwanza akizungumza na GB Pazzo (Kulia) kutoka Radio Metro na Mmiliki wa Mtandao huu.
Na:Binagi Media Group
Wananchi wa Mtaa wa Unguja Kata ya Mbugani Jijini Mwanza wamehimizwa kuzingatia kanuni za Usafi katika Mtaa wao ikiwa ni pamoja na kujiunga na Mfumo wa Majitaka ili kutotiririsha ovyo Majitaka.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mary Dismas Elias ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Afya katika Mtaa huo, wakati akizungumza na Mtaa kwa Mtaa, Kata Kwa Kata ambayo ni Kapeni ya Radio Metro juu ya adha za uchafu katika Mtaa huo.

Elias aliwahimiza wakazi wa mtaa huo ambao sehemu kubwa ni mwinuko kuepukana na tabia ya kuririsha ovyo majitaka yakiwemo ya Vyooni ovyo hususani wakati wa mvua badala yake wajiunge na mfumo wa majitaka ambao unatarajiwa kuwafikia hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Unguja Richard Daniel Kajuna alisema kuwa mpango wa kuwaunganisha wakazi wa mtaa huo katika Mfumo wa Majitaka imekwisha kamilika, ambapo takribani nyumba mia mbili zinatarajiwa kuunganishwa katika Mfumo huo.

Kajuna alibainisha kuwa utekelezaji wa mpango huo unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka MWAUASA kwa kushirikiana na Bank ya dunia pamoja na Shirikala la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makazi UN Habitat.


Wananchi wa Mtaa wa Unguja walielezea kufurahishwa kwao na mpango huo wa kuwaunganisha na mfumo wa majitaka ambapo wamebainisha kuwa wataondokana na adha kubwa waliyokuwa wakiipata hususani wakati wa mvua ambapo baadhi ya wakazi wa mtaa huo walikuwa wakitapisha majitaka ya vyooni na hivyo kuhatarisha afya zao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja Jijini Mwanza Richard Daniel Kajuna (Kushoto) akizungumza na GB Pazzo (Kulia) kutoka Radio Metro na Mmiliki wa Mtandao huu.
Wa kwanza Kulia ni GB Pazzo na wawili kushoto ni Julieth Kashaigili na Alphonce Tonny Kapela pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Unguja Kata ya Mbugani Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.