LIVE STREAM ADS

Header Ads

LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA MKOANI MWANZA.

Umati wa Wananchi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM waliojitokeza hii leo Jijini Mwanza kumlaki Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Mondule (CCM) Ndg.Edward Ngoyai Lowasa. Lowassa aliwasili Mkoani Mwanza kusaka sahihi za wadhamini kwa ajili ya kupata fursa ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
KWA MTAJI HUU JUHUDI ZA KUMKWAMISHA LOWASSA, NI JUHUDI ZA KUIANGUSHA CCM KATIKA UCHAGUZI MKUU MWEZI OCTOBA MWAKA HUU.
Picha zote na Malongo Mbeho
Umati wa Wananchi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza uliojitokeza Kumpokea Mbunge wa Jimbo la Monduli (CCM) na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa ambae baada ya Kutangaza nia ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kuchukua Fomu, ameanza harakati za kusaka sahihi za wadhamini ili kumwezesha kugombea nafasi hiyo.
Lowassa akiwasili katika Viwanja vya Gand Hall Jijini Mwanza
Umati wa Wananchi na Makada wa CCM wakiwa tayari kumpokea Ndg.Lowassa katika Viwanja vya Gand Hall Jijini Mwanza hii leo.

No comments:

Powered by Blogger.