KOTECHA AWAHIMIZA WANANCHI JIJINI MWANZA KUWA WATUNZAJI BORA WA MAZINGIRA.
Diwani wa Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza Bhikhu Kotecha
(Katikati) akizungumza katika Kilele cha Wiki ya Mazingira Jijini Mwanza hii
leo. Kushoto ni Afisa Mazingira Jiji la Mwanza Charles Amani na Kulia ni Mrashy
Diana Manyilizo ambae ni Mwenyekiti wa Asasi ya Uchungu na Mwana Mkoani Mwanza.
Na:Malongo Mbeho
Wananchi
wa jiji la Mwanza waehimizwa kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko.
Bhikhu Kotecha ambae ni diwani wa Kata ya
Nyamagana Wilayani Nyamagana alitoa ushauri huo hii leo katika kilele cha
maadhimisho ya wiki yamazingira duniani yaliyoadhimishwa katika bustani ya
TAMPERE iliyopo eneo la Makongoro Jijini Mwanza.
Kotecha alisema kuwa uhifadhi wa maji, ardhi na hewa hutasaidia
usalama wa afya ya binadamu na na hivyo kupunguza magonjwa hatarishi kama vile kipindupindu na kuhara husababishwa na
utunzaji mbovu wa mazingira.
Nae Charles Amani ambae ni afisa mazingira Jiji la Mwanza aliwahimiza
wananchi kuwa na desturi ya kutunza mazingira kwa kushirikiana na ofisi za
mazingira zilizopo katika maeneo yao
Amani alisema kuwa elimu ya
utunzaji wa mazingira inaendelea kutolewa kwa wananchi lengo likiwa ni kila
mmoja kutambua wa uhufadhi wa mazingira.
Wiki ya Mazingira Duniani ilianza kuanzimishwa tangu June Mosi
mwaka huu na kilele chake kikiwa ni hii leo juni tano ambapo kitaifa
maadhimisho hayo yamefanyiki mkoani Tanga kwa kauli mbiu isemayo NDOTO BILIONI
SABA DUNIA MOJA, TUMIA RASILIMALI KWA UANGALIFU kikiwa kimelenga kuwahimiza
wananchi kutumia rasilimali zilizopo kunendana na idadi ya watu iliyopo.
Kulia ni Afisa Mazingira Jiji la Mwanza Charles Amani na Kulia ni Mrashy Diana Manyilizo ambae ni Mwenyekiti wa Asasi ya Uchungu na Mwana Mkoani Mwanza akizungumza kwa niaba ya asasi zisizo za Serikali Mkoani Mwanza. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza Bhikhu Kotecha.
Maoni kutoka kwa wadau wa Mazingira yalitolewa pia
Maoni kutoka kwa wadau wa mazingira yakitolewa
Mazingira ni uhai
Wanafunzi nao walishirikishwa juu ya namna ya utunzaji wa mazingira ambapo pia walipata fursa ya kutoa maoni yao
Wadau wa Mazingira Mkoani Mwanza
Kilele cha Wiki ya Mazingira Jijini Mwanza
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Jijini Mwanza
SOMA BANGO HILO KWA UMAKINI.
KUONA SIKU YA UFUNGUZI BONYEZA HAPA
KUTAZAMA ILIVYOKUWA MWAKA JANA BONYEZA HAPA
No comments: