LIVE STREAM ADS

Header Ads

BALOZI LIBERATA MULAMULA AWAAGA TAMCO RASMI, ASEMA UMOJA WAO NI MFANO WA KUIGWA.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Watanzania DMV (TAMCO)Ustadh Ally Mohamed akimlaki Mhe.Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulaula mara tu alipowasili kwenye ukumbi wa park iliyopo Silver Spring, Maryland nchini Marekani alipokuja yeye Mhe. Balozi akiambatana na mumewe Eng.George Mulamula (hayupo pichani) na mwanae Alvin Mulamula (kulia) kujumuika na wanajumuiya hao katika futari ya pamoja na kutumia futari hiyo kuwaaga rasmi.

Imeandaliwa na Kwanza Production na Vijimambo Blog.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe.Liberata Mulamula jana jioni siku ya Jumapili July 12, 2014 alijumuika na wanajumuiya ya Kiislam ya DMV (TAMCO) katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na jumuiya hiyo.

Katika hotuba yake. Mhe.Liberata Mulamula aliwakumbusha kwa mara ya kwanza alipofika kulitumikia Taifa kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani , ambapo Jumuiya hiyo ndio iliyomkaribisha kwa mara ya kwanza hivyo kwa jana ilikuwa ni siku ya kuagana na jumuiya hiyo rasmi. 

Mhe.Liberata Mulamula aliwashukuru TAMCO kwa ushirikiano na mshikamano wao na kuzitaka Jumuiya zingine za Watanzania ziige mfano wao kwani TAMCO ni jumiya ya Kiislam iliyoimara, isiyotetereka na yenye uongozi makini. 

Mhe.Balozi Liberata Mulamula aliushukuru uongozi wa TAMCO kwa kumkaribisha ili kuzungumza na Watanzania wanajumuiya ya TAMCO ambapo alitumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.

Uongozi wa TAMCO ulimzawadia Mhe.Balozi Liberata Mulamula zawadi na yeye kutoa mchango wake wa mwaka kwa jumuiya hiyo inayo wakubali Watanzania wote bila kubagua rangi, kabila wala dini.
 Mtunza fedha msaidizi wa TAMCO. Bi. Asha Hariz(kushotao) akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula kuelekea ukumbini siku ya Jumapili July 12, 2015 siku Mhe. Balozi alipopata mwaliko wa Jumuiya hiyo wa kufuturu pamoja na kuwaaga rasmi.
Mwenyekiti wa TAMCO ustadh Ally Mohamed akiongea machache na baadae kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea na wanajumuiya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Wanajumuiya wa TAMCO na kuwaaga rasmi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akikabidhi mchango wake wa TAMCO wa mwaka kwa mtunza fedha msaidizi ustadh Shamis Abdullah.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.

Picha ya pamoja

No comments:

Powered by Blogger.