LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YATAKIWA KUTOA ELIMU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWA WAKULIMA WA KANDA YA ZIWA.

Kilimo cha zao la Pamba
Na:Shaban Njia
Serikali imetakiwa kutoa Elimu ya Kilimo cha Umwagiliaji kwa Wakulima wa zao la Pamba hapa nchini ili kuwaondolea adha ya kutegemea Mvua za masika ambazo zimekuwa zikiwasababishia hasara kutokana na kutokidhi katika ulimaji wa zao hilo.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Kampuni ya NIDA TEXTILE iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Akbar Mohamed wakati akizungumzia kilimo cha zao la pamba kwa msimu wa mwaka 2015/2016.

Alisema Serikali inapaswa kuelekeza nguvu kwa wakulima katika kuwaelimisha juu ya kulima kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kupunguza athari za ukosefu wa mvua katika kilimo hususani katika zao la pamba ambalo uzalishaji wake umepungua kwa kiasi kikubwa.

Mohamed ambaye pia Kampuni yake ni Mwanachama wa Umoja wa Makampuni yanayochambua Pamba Mkoa wa Shinyanga (UMWAPA), alisema kuwa kwa sasa umoja huo unawadai wakulima wa Pamba kiasi cha shilingi Bilioni 4.7 kwa ajili ya Madeni ya pembejeo za Kilimo kwa mwaka 2014/2015 hali ambayo ulipaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana na wakulima kutopata mavunoi ya kutosha katika msimu uliopita.

Aliitaja Mikoa ambayo imekuwa kinara wa Madeni hayo kuwa ni pamoja na Geita, Shinyanga hususani Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Mwanza katika Wilaya ya Sengerema na kuongeza kuwa inahitajika nguvu kubwa ili wakulima wa maeneo hayo waweze kulipa madeni hayo kwa wakati.

"Serikali ielekeze nguvu kwa wakulima katika kuwaelimisha juu ya kulima kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kupunguza hatari ya ukosefu wa mvua inayojitokeza na kuhatarisha kilimo cha zao la pamba kama inavyotaka kujitokeza kwa Mwaka huu".Alisema Mohamed.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Kahama Oil Mill, William Matonange alisema kuwa katika kipindi cha msimu wa Pamba kwa mwaka huu Makampuni ya ununuzi yanakabiliwa na changamto nyingi ikiwemo ile ya upungufu wa mavuno ya zao hilo pamoja na Pamba kuendelea kuchanganywa na maji ili kuiongeza uzito.

"Lakini pia Serikali kupunguza kodi ya huduma kwa makampuni ya ununuzi wa pamba kwani Makampuni hayo yamekuwa yakikopesha Pambejeo pasipo kuwa na riba yoyote kwa Wakulima wa zao hilo hali ambayo inawatia hasara katika ununuzi". Aliongeza Matonange.

No comments:

Powered by Blogger.