LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA SOKA YA STANVIC YAZAWADIWA POINTI TATU MUHIMU KATIKA MICHUANO YA BULABO CUP JIJINI MWANZA.

Na:Oscar Mihayo
Timu ya Stanvic imejinyakulia pointi tatu muhinu za mezani baada ya timu ya The winning Star kutofika uwanjani bila taarifa yoyote katika Michuano ya  Bulabo Cup ilioanza kutimua vumbi hapo jana katika uwanja wa shule ya sekondari Mahina Jijini Mwanza.

Mratibu wa mashindao hayo Bulabo Paschal ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa Mahina Kati alisema kuwa anasikitika kuona vijana wanasusia mashindano hayo wakati yanatumia gharama kubwa kwenye uandaaji wake ambapo aliwataka kushiriki kwa moyo mmoja ili kufanikasha lengo lake.

“Haya mashindano lengo lake kubwa ni kuibua vipaji ikiwa ni pamoja na kuwaandalia ajira vijana kupitia michezo, lakini pia kuwaepusha na makudi mabovu hivyo kutoleta timu uwanjani ni picha mbaya”. Alisema Bulabo.

Aidha alibainisha kuwa mashindano ambayo yanashirikisha timu 30 yanayotarajia kufikia tamati julai 25 mwaka ambpo bingwa ataibuka na kikombe chenye thamani ya shilingi Laki mbili (200,000) na fedha taslimu pia shilingi Laki mbili (200,000), mshindi wa pili nae shilingi Laki mbili (200,000) huku mchindi wa tatu akiibuka na shilingi Laki Moja (100,000).

Aliongeza kuwa timu bora itajinyakulia shilingi elfu Kumi (10,000), huku pia mchezaji bora, timu yenye nidhamu, kocha bora na kipa bora wote kwa kila mmoja akijinyakulia kiasi kama hicho cha fedha..

Kwa upande wake Mwenyeki wa mashindano hayo Soga Bagetsoga aliwata washiriki kujiandaa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuonyesha soka la kuvutia huku akiwasihi kutumia michuano hiyo kama mabalozi wazuri wa kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

No comments:

Powered by Blogger.