LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU ZITAKAZOSHIRIKI MICHUANO YA U-17 YA AIRTEL RISING STAR 2015 MKOANI MWANZA ZATAJWA.

Aliesimama ni Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) Nasib Maburuki akizungumza katika Ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star mwaka jana katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.
Na:Oscar Mihayo
Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) kupitia kamati kuu ya soka la vijana Mkoa imeziteua timu sita za wavulana na wasichana ili kushiriki michuano ya Airtel Rising Star chini ya miaka 17 (U-17).

Akizungumza na Binagi Media Group, Katibu Mkuu wa chama hicho Nassib Mabrouk
alizitaja timu shiriki kuwa  ni Alliance Sports Academy,Gold Sports Academy na Misungwi Academy kwa upande wa Wavulana.

Nyingine ni Marsh Academy, TSC Academy na Alliance Academy kwa Wasichana na kusema kuwa michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Julai 20
mwaka huu.

Mabrouk alizitaka timu zilizoteuliwa kuwakilisha mkoa Mwanza kuhakikisha zinaanza usahili wa wachezaji wake 20 mapema kabisa ikiwa na kufuata vigezo vya mashindano hayo kwani hawataki mamluki katika michuano hiyo na kwa watakaofanya hivyo watapewa adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufungiwa miaka mitatu kutojihusisha na soka.

“Tunaomba timu zote ziwatumie wachezaji wenye vigezo ikiwa ni pamoja na kutumia vyeti vyao vya kuzaliwa pamoja na TSM9 ya shule anayosoma ili kujilidhisha na umri sahihi wa wachezaji watakaoshiriki mashindano hayo”. Alisema Mabrouk.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa kila timu imeisha kabidhiwa vifaa vya michezo ambavyo ni jozi mbili za jezi na mipira miwili na hivyo kuzikata timu shiriki kufanya maandalizi ya kutosha mapema ili kufanya vizuri katika michuano hiyo na kuleta heshima ya soka Mkoani Mwanza.


Tazama HAPA Picha za Uzinduzi wa Michuano hiyo mwaka jana.

No comments:

Powered by Blogger.