LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOKO LA WAKULIMA KAHAMA MKOANI SHINYANGA LATEKETEA KWA MOTO.

Na:Shaban Njia
Moto mkubwa uliozuka katika soko la Wakulima Mjini Kahama Mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia jana umeweza kuteketeza bidhaa mbalimbali zilizokuwa katika eneo hilo na kusababisha hasara kubwa kwa kulima na wafanyabiashara wa eneo hilo.

Akiongea leo na Binagi Media Group, Meneja wa Soko hilo Machimu Nelson alisema kuwa moto huo ulianza majira ya saa nane za usiku wa kuamkia jana huku mashuhuda wa tukio hilo wakidai kuwa chanzo kikuu cha moto huo ni hitilafu iliyojitokeza katika mita ya umeme na hivyo kusababisha mlipuko mkubwa katika soko hilo.

Nelson Alisema kuwa baada ya kutokea kwa moto huo wasamaria wema waliamua kupiga simu kwa Jeshi la zima moto Wilayani Kahama na hivyo kuwahi katika eneo hilo la tukio japo moto ulikuwa tayari umesambaa kwa kasi katika soko hilo kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma maeneo hayo.

Hata hivyo Meneja huyo alisema kuwa baada ya kupiga siku zima moto jeshi hilo liliwasili katika eneo la tukio kwa wakati na kuongeza baada ya jitihada za kuzima moto kuendelea katika eneo pia waliweza kupata msaada wa kikosi kingine cha zima moto kutoka katika Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Buzwagi na hivyo kuweza kuuzima majira ya saa mbili za asubuhi jana.

Mmoja wa Wafanyabiashara ambao bidhaa zao ziliteketea kwa moto katika tukio hilo Wanne Joakimu alisema kuwa ameunguliwa mabanda mawili ambayo yalikuwa na bidhaa za Maparachichi na Ndizi na kufafanua kuwa amepata hasara takribani milioni tatu.

Joakimu alisema kuwa kutokana wafanyabiashara wengi katika soko hilo kufanya biashara kutokona na Mikopo kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha, ameiomba Serikali kuwasaidia ili waweze kupata stahiki zao za msingi ikiwemo kulipwa fidia za bidhaa zao.

Kwa upande wake Sajenti US/ZM 2592 Erick Malali kutoka Kikosi cha zima moto Halmashauri ya Mji wa Kahama, aliwataka Wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanakuwa vyeti vya Kikosi hicho ili kuwa rahisi wanapopatwa na majanga ya moto iwe rahisi kusamehemewa madeni wanayokuwa nayo katika taasisi za kifedha.

Pia Malali alisema kuwa ni vyema sasa kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama kuhakikisha kuwa wanatengeneza miundombinu mizuri ya barabara hasa katika masoko kutokana na kukumbana na changamoto nyingi wakati wa majanga ya moto kutokana na ubovu wa miundombinu.

Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) Wilaya ya Kahama Sulle Khabati alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia tuhuma za hitilafu ya umeme zinazodaiwa kusababisha moto huo, alijibu kwa ufupi kupitia ujumbe wa maneno kuwa yupo darasani kwa ajili ya mafunzo.

No comments:

Powered by Blogger.