LIVE STREAM ADS

Header Ads

HII NI MAALUMU KWA AJILI YA WAKAZI WA WILAYA YA BUNDA MKOANI MARA KATIKA SIKU YA IDD MOSI.

Soma bango kwa Umakini zaidi.
91.7 Mazingira Fm Radio kwa kushirikiana na DP Consult Company Limited wanawaletea burudani kabambe wakazi wa Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na viunga vyake siku ya Idd Mosi.

Atakuwepo Msanii Bob Haisa kutoka Mwanza akisindikizwa na Wasanii Busy F, Nelly Mjaluo, Esther Maarifa pamoja na wadada machachari wa kunengua viuno waitwao Bai Koko.

Kumbuka burudani hii itadondoshwa katika Ukumbi wa Serengeti Resort kwa mtonyo nafuu kabisa wa buku tano kwa watu wazima kuanzia saa mbili za usiku hadi majogoo ambapo kwa watoto itakuwa buku moja tu kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni. 

Hakika burudani hii si ya kukosa maana ukiikosa utajutia hadi mwaka ujao hivyo mimi, wewe na yule tukutane ndani ya Serengeti Resort Bunda siku ya Idd Mosi bila kukosa ili tusherekee siku kuu ya Idd pamoja.

Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

No comments:

Powered by Blogger.