LIVE STREAM ADS

Header Ads

BUGUKU AELEZA KILICHOMSUKUMA KUTIA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA BUHONGWA JIJINI MWANZA.

Na:Oscar Mihayo
Baada ya kujitosa kuwania kuteuliwa na chama chake ili kugombea udiwani Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguku (CCM) katika Kata hiyo Maduhu Sultan ameeleza sababu zilizomsukuma kugombea.

Akizungumza hivi karibuni na Binagi Media Group, Sultan alibainisha kuwa ameamua kuwania nafasi hiyo baada ya kuombwa sana na wananchi wa kata hiyo.

"Kutokana na juhudi nilizozifanya katika uongozi wangu wa kuwa mwenyekiti wa mtaa wa Buguku, ambazo ni pamoja na kutekeleza ahadi nilizoziahidi kwa muda mwafaka ambazo ni pamoja na ujenzi wa ofisi ya mtaa wangu pamoja na kusimamia ujenzi wa mabomba ya maji safi na hivyo kuondoa kero zilizokuwepo hapo awali, wananchi wameniomba kugombea udiwani katika Kata hii ili niendelee kushirikiana nao kwa ajili ya maendeleo zaidi ya Kata yetu". Alieleza Sultan.

Mchakato wa Watia nia ya Kugombea Ubunge na Udiwani ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM kujinadi kwa wanaccm katika Kata zote Wilayani Nyamagana bado unaendelea ambapo mbivu na mbichi za kuwajua watakaopitishwa kugombea zitajulikana Octoba Mosi mwaka huu ndani ya chama hicho.
Powered by Blogger.