LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, VIJANA NCHINI WAPEWA SOMO.

Na:Oscar Mihayo
Vijana nchini wametakiwa kuwa makini katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini kwa kuchagua viongozi waadilifu na wazalendo bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.

Pia wametakiwa kuwachagua viongozi wanaojua shida na matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumika kisiasa.

Rai hiyo ilitolewa wikendi iliyopita katika mdahalo maalum wa vijana wa Kata ya Mkuyuni Jijini Mwanza ambao ulihusisha jinsia na rika zote kutoka katika Kata hiyo.

Mwenyekiti wa mdahalo huo John Paskal alisema lengo la mdahalo huo ni kutoa semina elekezi ya kumchagua kiongozi anaefaa ambaye atashirikiana na wananchi katika kutatua kero zinazowakabiri.

“Tuanataka kiongozi anayejua shida zetu na atueleze ni kwa namna gani atazitatua endapo kama akipewa dhamana ya kuwa kiongozi na sio kutudanganya na maneno matamu yasiyo tekelezeka”. Alisema Paskal.

Kijana John Jonas alisema kuwa kama vijana watafanya siasa za ushabiki au siasa za kuwagawa kikabila, hali inaweza kuwa mbaya kiusalama ambapo aliwahimiza vijana wenzake kusimama imara katika kusikiliza sera za wagombea pindi wawapo majukwaani kabla ya kufanya maamuzi ya kuwapigia kura.

Kijana Mwingine Bakari Mustapha aliwataka vijana wenzie kuwa waangalifu kwa viongozi wanaowachagua ili wasi jutia pindi watakapokuwa wamemchagua kiongozi ambae hawajibiki kwa wananchi waliomchagua.

Nao vijana wengine waliokuwa wakichangia katika mdahalo huo walisema kuwa, vijana ambalo ni kundi kubwa linalotegemewa katika mabadiliko ya kijamii wanapaswa kujitambua kwanza ndipo wanaweza kukaa na kutafakari ni kiongozi yupi wamtakae bila kufuata ushabiki wa vyama ambao hauna tija.
Powered by Blogger.