LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA MAJOWA SECURITY AJITOSA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MKUYUNI JIJINI MWANZA.

Judith Ferdinand
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya  Majowa Security Guard ambae pia ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency ACT Wazalendo Kata ya Mkuyuni Jijini Mwanza Masatu Wasira jana amerudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Udiwani wa kata hiyo kupitia chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kurudisha fomu, Wasira alisema kuwa lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni kupigania maendeleo ya Kata ya Mkuyuni kutokana na kata hiyo kuwa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na Kata jirani.

Wasira alisema kuwa kama chama chake kitampa ridhaa ya kugombea na hatimae kuchaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo atayapa kipaumbele mambo mbalimbali ikiwemo kushughulikia changamoto ya ukosefu wa maji pamoja na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa inayowokabili wakazi wengi katika Kata hiyo.

Pia alisema atashirikiana na viongozi wa elimu pamoja na wazazi katika kutaua changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaosoma katika shule zilizopo ndani ya kata hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba zinapatiwa kupatiwa vitendea kazi vya kutosha.

Wasira alisema kuwa viongozi waliopita waliahidi kuwaletea zahanati wakazi wa kata hiyo ila mpaka sasa ni zaidi ya miaka 20 ahadi yao hawaijatekeleza.  

Aidha alisema kuwa ataanzisha ligi za michezo ya aina mbalimbali katika kata hiyo, ili kuinua na kuibua vipaji na hatimae kuwa sehemu ya ajira kwa vijana.

Mbali na Wasira kuna jumla ya watia wanne waliochukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya kugombea udiwani Kata ya Mkuyuni kupitia chama cha ACT Wazalendo ambao ni Abasi Kapehe, Ibrahim Mgusi na Emmanuel Daudi ambapo watatu tayari wamerudisha fomu zao huku mmoja akitarajiwa kurudisha fomu yake hii leo julai 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya zoezi la kurejesha fomu ndani ya ACT Wazalendo.
Powered by Blogger.