LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALI SI SHWARI NDANI YA CCM. LEMBELI AJIUNGA NA CHADEMA WENGINE NAO KUFUATA NYAO.

James Lembeli
Na:Binagi Media Group
Mtikisiko wa Kisiasa umeendelea kukitesa Chama cha Mapinduzi CCM, kufuatia kuwepo kwa kasi ya Makada wake kujiunga na vyama vya Upinzani kwa huku sababu kubwa zikielezwa kuwa ni haki kutotendeka katika kinyang'anyiro cha kumsaka mgombea wake wa urais pamoja na kukithiri rushwa na ufisadi katika chama hicho.

Siku chache zilizopita zaidi ya wanazuoni 30 wa chama hicho Jijini Dar es salaam pamoja na waliokuwa madiwani na wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilayani Monduli walijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na hivyo kuonyesha hali ilivyo tete ndani ya chama hicho.

Wakati hali ikiwa hivyo, hii leo pia Mbunge wa Jimbo la Kahama Mkoani Shinyanga James Lembeli (CCM), ametangaza rasmi kujiunga na Chadema ambapo ameeleza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa ndani ya CCM.

Ameyasema hayo katika Makao Makuu ya Chadema na kuongeza kuwa CCM imekuwa na matukio ya rushwa ambayo ni pamoja na Wanaccm kununuliwa kadi za chama na kupewa rushwa wawania Ubunge huku kukiwa hakuna hatua zozote zinachukuliwa licha ya yeye kuripoti vitendo hivyo katika ngazi zinazohusika.

"Mwaka 2010 nilidanganywa na viongozi wangu kuwa nigombee ubunge katika Jimbo la Ushetu ambalo halikuwepo na hii inaonyesha kwamba nilikuwa sihitajiki ndani ya chama changu". Alisema Lembeli.

Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii katika bunge linaloelekea ukingoni, ameongeza kuwa sababu nyingine iliyomlazimu kuihama CCM ni pamoja na kutoridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea urais namna ulivyoondeshwa.

Hata hivyo Lembeli ametanabaisha kwamba atagombea ubunge kupitia Jimbo la Kahama Mjini kwa tiketi ya Chadema baada ya kuombwa na wananchi wa jimbo hilo kuwatumikia.


Wakati hayo yakiendelea kushika kasi kubwa katika duru za siasa nchini, pia kuna idadi nyingine ya Makada wa CCM wanaotajwa kwamba huenda nao wakajiunga na vyama vya Upinzani.

Wanaotajwa ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Mara Esther Bulaya ambae anatajwa kuwa huenda akajitoa ndani ya chama chake kufuatia kuwekewa ngumu katika kugombea ubunge Jimbo la Bunda Mjini kwa minajiri ya kumuachia Mh.Steven Masatu Wasira na mwingine akiwa ni Mh.Edward Lowasa ambae inaelezwa kuwa mambo yasipowekwa sawa nae atatimkia upinzani kufuatia jina lake kukatwa katika harakati za kumpata mgombea ndani ya chama chake.
Powered by Blogger.