WAZEE WA KATA YA MBUGANI JIJINI MWANZA WAHIMIZA USHINDI NA MSHIKAMANO NDANI CCM.
Kikao cha Wazee na Vijana wa CCM Kata ya Mbugani Jijini Mwanza kilichokutana jana Aspen Hotel ili kutafuta Mshikamano ndani ya Chama chini ya Uongozi wa Wazee wa Kata hiyo.
Na:George GB Pazzo
Uongozi
wa Wazee wa Kata ya Mbugani Jijini Mwanza umewahimiza Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Kata hiyo kuondoa tofauti zao za Kisiasa na badala yake
waungane kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa chama hicho kinaibuka na ushindi katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Uongozi huo ulitoa kauli hiyo jana
kupitia kwa Mwenyekiti wake Mzee Joseph Daniel katika kikao kilichofanyika
Aspen Hotel Jijini Mwanza, kikiwa kimewakutanisha Wazee pamoja na Vijana wa CCM
kutoka Kata hiyo ya Mbugani.
Mzee Daniel alisema kuwa mshikamano ndani ya
CCM katika Kata hiyo umepotea, hali ambayo ilipelekea chama kupotea ushindi
katika Uchaguzi wa Mwaka 2010 na hivyo kuwachanganya wanaccm hususani Wazee wa
Chama.
Alisema baada ya hali hiyo kujitokeza,
Wazee na Vijana wa CCM Kata ya Mbugani waliamua kutafuta mshikamano ndani ya
Chama kupitia kwa Uongozi huo wa Wazee wa Kata ya Mbugani.
“Mshikamano ndani ya chama hivi sasa
haupo na hali hii imepelekea Kata yetu kupoteza udiwani na hivyo kuongozwa na
upinzani. Ni kutokana na hilo, wazee wa CCM na Vijana wa CCM wameamua kutafuta
mshikamano ndani ya chama ili kuhakikisha umoja unaimalika na kukiwezesha chama
kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu kwa ngazi ya Udiwani, ubunge
pamoja na Urais”. Alisema Mzee Daniel ikiwa ni nukuu aliyoisoma kutoka katika
barua iliyoandikwa na Wazee na Vijana wa CCM Kata ya Mbugani.
Kwa pamoja kikao hicho kupitia kwa
wachangiaji mbalimbali akiwemo Mzee Benedict Pamba, Aman Mussa, Ally Kashumali,
Halima Mbomba na Vijana Ally Msoya, Adroph Charles, Shaban Majuto, Mohamed
Khamis pamoja na Faustine Atanas kiliazimia kwamba Umoja na Mshikamano ndani ya
CCM vinapaswa kuimalishwa ili kuhakikisha kwamba chama kinarudisha heshima yake
kwa kuibuka na ushindi katika Uchaguzi wa Mwaka huu.
Kutoka Kushoto ni Faustine Atanas ambae ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mbugani, Katikati ni Joseph Daniel ambae ni Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Mbugani na Kulia ni Ally Kashumali ambae ni Katibu wa Wazee Mbugani.
Wazee Kata ya Mbugani
Mzee Kata ya Mbugani akitoa Mawazo yake ya kuimarisha Umoja ndani ya CCM.
Kijana Kata ya Mbugani akitoa Mawazo yake ya kuimarisha Umoja ndani ya CCM.
Kijana Kata ya Mbugani akitoa Mawazo yake ya kuimarisha Umoja ndani ya CCM.
Kijana Kata ya Mbugani akitoa Mawazo yake ya kuimarisha Umoja ndani ya CCM.
Kijana Kata ya Mbugani akitoa Mawazo yake ya kuimarisha Umoja ndani ya CCM.
Mzee Kata ya Mbugani
Mzee Kata ya Mbugani
Wazee na Vijana Kata ya Mbugani
Wazee na Vijana Kata ya Mbugani
Wazee Kata ya Mbugani
Wanahabari
Ahsante Kwa Kutembea Mtandao Wetu, Endelea Kuwa Nasi.