LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: "UMUHIMU WA KUFUATA NDOTO YAKO" SEHEMU YA KWANZA.

Ndoto ni tukio la kubuni ambalo linaonekana kwenye akili wakati mtu kalala. Sasa waweza kupata njozi yako mchana au usiku wakati umelala. Wanasaikolojia wengi wanaamini ndoto nyingi ambazo watu wanaota usiku ni matokeo ya kile walichosikia au kukifanya au kukisema mchana.
Njozi/Ndoto nyingi ambazo zinakuwa na manufaa na ukweli ndani yake ni zile mtu anazozipata mchana kweupe pale anaposafisha akili yake na kuiacha safi ndipo anaanza kupata picha fulani katika akili yake. Anajiona anatengeneza au anafanya jambo fulani kubwa.
Kila kitu kimeanzia kwenye ndoto, mtu alikiona katika akili yake kama picha fulani maana binadamu anafikiri kwa picha ndipo akaanza kukifanyia kazi kwa umakini pasipo kukata tamaa na leo tunakiona kama kitu kilichokamilika.
Hebu fikiria mambo ambayo Edison alifanya alikuwa na ndoto ya kutengeneza bulbu japo alifeli zaidi ya mara 9000 katika kutengeneza balbu ya umeme, lakini hakukata tamaa na kuna wanahabari walimfuata wakamuuliza mbona lakini hakukata tamaa maana alifeli mara nyingi sana ila yeye aliwaambia sikufeli bali niligundua njia zaidi ya 9000 ambazo bulbu isingeweza kubadilika.
Mara nyingi watu wanaokuwa na ndoto huwa wanataka kubadili dunia na kufanya mambo ambayo yatabadilisha sio maisha yao tu bali kufanya dunia na watu wote kufurahia kile walichokigundua, kwa maana hii ninaweza kusema kwamba watu wenye ndoto huwa ni wajasiriamali na sio wafanyabiashara.
Ni rahisi kumsahau mfanyabiashara pindi atakapokufa lakini mjasiriamali ni vigumu kumsahau maana mjasiriamali huwa nia yake kubwa katika maisha sio hela ila ni kufanya kitu ambacho kitaacha doa na kubadilisha maisha ya watu hata kama hatopata hela, japokuwa fedha huwa zinawafuata baada ya kufanikiwa katika suala hilo ambalo wanalifanya. Leo hii hatuwezi msahau Edison maana alikuwa mjasiriamali hivyo jifunze tofauti kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara.
Hebu fikiria mtu kama Marconi, alibadilisha dunia nzima katika suala la mawasiliano kwenye redio na Tv, ni mvumbuzi wa teknolojia ya mawasiliano pasipo waya katika redio na baadae walitumia njia hiyo hiyo kuweka mawasiliano katika Tv pasipo waya.
Nataka nikuambie mtu mwenye ndoto fulani ni yeye tu huwa anaiona katika akili yake watu wengine wanaweza wasimuelewe kile anachokisema, niliwahi kusoma habari ya Marconi wakati amekuja na hii ndoto watu walimuita ni mtu mwenye matatizo ya kiakili na ilibidi apelekwe kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili ili kuangalia akili yake kama ilikuwa ina matatizo lakini alikutwa mzima na baba yake mara kadhaa alikuwa akimkatisha tamaa kwamba anapoteza muda kwa kile anachokifanya. Ila baada ya muda alitimiliza ndoto yake.
Alexander Graham Bell alibadilisha dunia katika suala la simu, alikuwa na hii ndoto na mara kadhaa alikuwa akijiona anaongea na mtu ambae yupo sehemu nyingine kisha akaanza kutendea kazi, leo hii tunapiga simu marekani,china,india tukiwa hapa hapa kwetu.
Pasipo watu kama hawa Edison, Marconi, Bell , wright Brothers kusimamia ndoto zao na kuhakikisha kile walichokuwa wanakiona kwenye akili zao wanakitendea kazi sijui dunia imekuwaje leo.
Na unaweza kuona baada ya wao kufanyia kazi ndoto zao kila mtu kanufaika, wamebadili mfumo duniani kote hawa ndio baadhi ya wajasiriamali maarufu duniani na wengine wengi waliokuja baada yao.
Asante Mungu kwa kuwaumba na naomba wapumzishe kwa amani wote hawa waliofanya mambo makubwa katika dunia hii na kubadilisha maisha ya kila anayeishi katika dunia hii.
Ni dhahiri kwamba wewe na mimi hatuna tofauti na wao, hahahaahahah ndio, hatuna tofauti kabisa tofauti iliyopo ni namna tu unavyojichukulia wao walijiona ni watu ambao wanaweza kutimiliza ndoto zao na wakazifanyia kazi na bahati nzuri pia wewe na mimi tunazo ndoto mbalimbali.
Nataka ukaanze kutendea kazi ile ndoto yako uliyokuwa umeikatia tamaa kuitenda, sema kabisa nipo hai sijafa na nitapambana, jua kabisa unao uwezo wa kuitimiza na wewe ukaweka doa jema katika dunia hii na kubadilisha maisha ya watu wote, na kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ambayo kila mtu ataifurahia.
Itaendelea
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
Email:allnhumph@gmail.com Phone: 0689 45 26 70/0765 53 68 42
Powered by Blogger.