LIVE STREAM ADS

Header Ads

JOHN BUYAMBA AAHIDI NEEMA JIMBONI ILEMELA AKIPATA RIDHAA YA KUWA MBUNGE 2015.

Na Neema Emmanuel
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Buyamba, amechukua fomu rasmi ya kuomba kupitishwa na chama hicho ili kuwania Ubunge jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza.

Akizungumza jana mara baada ya kuchukua fomu, Buyamba alisema amefikia uamuzi huo bila kushinikizwa na mtu ikiwa ni ridhaa yake mwenyewe yenye lengo la kuihamasisha jamii na kwa ajili ya kuleta maendeleo  ndani ya jimbo hilo.

Alisema akipitishwa na chama kuwania nafasi hiyo kuna mambo mengi anatarajia kuyafanya ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wananchi katika kutatua kero zinazoikabili Wilaya ya Ilemea ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara, afya na elimu.

Buyamba alisema kuwa sifa na dhamira ya uongozi ni utumishi wa umma, hivyo yuko tayari  kuwatumikia wananchi bila ubaguzi ikizingatiwa kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama ikiwemo kuwa Kamanda wa UCCCM wilaya ya Misungwi.

Pia ni Mjumbe wa baraza la Mkoa katika jumuiya ya vijana wa CCM UVCCM Mkoa wa Mwanza, Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa na wilaya ya Ilemela ambapo nje ya siasa ni mjasiriamali mwenye elimu ya Chuo kikuu.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, aliwashauri watia nia wote wa ngazi mbalimbali katika jimbo la Ilemela kutokuwa na siasa za kuchafuana bali wazingatie taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa na chama.

Tazama Picha HAPA

No comments:

Powered by Blogger.