LIVE STREAM ADS

Header Ads

KANGE AAHIDI MABADILIKO KATA YA NYAMANORO WILAYANI ILEMELA IKIWA ATAPATA RIDHAA 2015.

Na Neema Emmanuel
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (28) amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimpitishe kuwania Udiwani wa Kata ya Nyamanoro.

Akichukua fomu jana katika Ofisi za Kata ya Nyamanoro, Kange alisema kuwa dhumuni lake kubwa la kuwania udiwani ni kuwatumikia wananchi na kushirikiana nao  katika mambo mbalimbali ya maendeleo.

Alisena ni  wakati muafaka kwa wanachama kuwa na imani naye, wampigie kura ili apeperushe bendera ya chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na hatimae kufanikisha pia ushindi kwa chama chake.

Kange alisema kuwa vipaumbele vyake vitakuwa katika sekta ya miundo mbinu, maji, huduma za afya na ajira, hivyo kata yaNyamanoro inahitaji kiongozi makini ambae ni yeye.

Ana nyadhfa mbalimbali ndani ya chama ambazo ni pamoja na kuwa Mwenyekiti UVCCM Kata ya Nyamanoro, Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Mwanza na Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM Taifa.

Nje ya siasa Kange ni Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali  la utoaji elimu ya matumizi ya dawa za kulevya na ujasiriamali Mkoani Mwanza liitwalo Mwanza Youth Organization ambae amebobea katika ufundi wa umeme wa magari.

Nae Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Ramadhani, aliwataka wagombea wote waliojitokeza kuchukuwa fomu kuzingatia kanuni na katiba ya chama katika harakati zake za kuwania uongozi kwa kuwa atakaenenda kinyume atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Tazama Picha HAPA

No comments:

Powered by Blogger.