LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOMEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI AAHIDI NEEMA KWA WANYONGE JIMBONI HUMO.

Muwania kuteuliwa Kugombea Ubunge Jimbo la Kahama Mjini (CCM) Seetbat Nkuba (Kushoto) akiwa na Mkewe (Kulia).
 Na:Shaban Njia
Mtangaza nia ya kugombea kiti cha Ubunge katika jimbo jipya la Kahama mjini Seetbat Nkuba, amesema kuwa iwapo kama chama cha Mapinduzi (CCM) kitampa ridhaa ya kugombea kiti cha Ubunge katika jimbo hilo na hatimae kuchaguliwa na wananchi kuwa mbunge, atahakikisha kuwa kunakuwa na dawati na Wanasheria katika ofisi yake kwa ajili ya kuwatetea wanyonge wanaopoteza haki zao kwa kukosa msaada wa kisheria.
Nkuba aliyasema hayo juzi katika ofisi za CCM Wilaya ya Kahama muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo jipya Kahama Mjini ambapo aliongeza kuwa kutoka na wananchi wengi kutokujua haki zao atalazimika kuunda kitengo hicho katika ofisi yake iwapo kama atapata ridhaa ya kuwa mbunge.
Mgombea huyo ambaye pia ni Mwanasheria wa kujitegemea alisema kuwa kwa sasa Wananchi wengi wamekuwa wakionewa kutokana na kutokujua sheria hali ambayo inafanya wengi kukosa haki zao za msingi za kisheria pindi wanapopata matatizo mbalimbali.
Alisema kuwa mbali na kutoa msaada huo wa kisheria kwa Wananchi pia alisema kuwa kama atapata ridhaa ya kuongoza Wananchi wa Jimbo la Kahama Mjini pia atahakikisha kuwa anainua uchumi wa mtu mmoja mmoja ili kuleta mabadiliko kutoka na Wilaya ya Kahama kwa sasa kuwa katika hadhi ya Manispaa.
“Ni lazima tuwe na chuo kikuu katika Manispaa yetu ili watoto wetu waweze kupata Elimu ya juu kwa karibu na hivyo kuongeza wasomi zaidi katika Manispaa yetu ambayo inazidi kukua kwa kasi katika maendeleo.” Alisema Nkuba.
Katika Kinyang’anyiro cha kuchukua fomu za kugombea kiti cha Ubunge katika majimbo matatu ya uchaguzi katika Wilaya ya Kahama mpaka kufikia juzi jumla ya Wagombea 12 tayari walikuwa wamechukua fomu katika majimbo ya Ushetu, Kahama Mjini pamoja na Msalala.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama Alexandrina Katabi aliwataja waliochukua fomu katika jimbo la Kahama Mjini kuwa ni Adamu Ngalawa ambaye pia ni katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Deogratius Mpagama, Sweatbat Nkuba, Deogratis Sazia, John Nyenye pamoja na Michael Bundala.
Waliochukua fomu katika Jimbo la Msalala ni pamoja na Emanuel Kipole ambaye ni mhadhiri chuo kikuuu cha Mlimani Dar es Salaam, Ezekiel Maigi anayeteteakiti chake, John Sukili pamoja na Nicholous Mabula huku katika jimpya la Ushetu wagombea wakiwa ni pamoja na Elias Kwandikwa ambae ni mhasibu kutoka ofisi ya (CAG) pamoja na Isaya Simon Bukhakie.
Muwania kuteuliwa Kugombea Ubunge Jimbo la Kahama Mjini (CCM) Seetbat Nkuba

No comments:

Powered by Blogger.