LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA AJITOA KUGOMBEA UBUNGE DAKIKA TATU BAADA YA KUCHUKUA FOMU.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza juzi na Wanahabari baada ya Kuchukua Fomu ya Kuwania kuteuliwa na Chama chake ili kupata ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Kahama Mjini Mkoani humo.

Hata hivyo maajabu katika maamuzi ya Mgeja yalijitokeza ndani ya dakika tatu mara baada ya kuchukua fomu hiyo ambapo alijitoa katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania kuteuliwa na chama chake ili ambapo ridhaa ya kugombea katika Jimbo la Kahama Mjini.

Fomu za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi nchini zilianza kutolewa kuanzia Julai 15,2015 na zilifikia tamati jana Julai 19,2015 majira ya saa Kumi alasiri.
Na:Shaban Njia
Mwenyekiti wa CCM Mkoani Shinyanga Khamis Mgeja akiwa katika Ofisi za Chama hicho Wilaya ya Kahama kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama chake ili apate ridhaa ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kahama Mjini ambapo hata hivyo alijitoa katika kinyang'anyiro hicho ndani ya dakika tatu mara baada ya kuchukua fomu.

Kujua waliochukua fomu bonyeza HAPA

No comments:

Powered by Blogger.