LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATIA NIA 24 KUCHUANA MAJIMBO MATATU WILAYANI KAHAMA HUKU KITENDAWILI KIKIWA NI KWA LEMBELI NA MGEJA.

Na:Shaban Njia
Zoezi la kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika majimbo matatu ya wilaya ya Kahama mkoani shinyanga, limemalizika jana huku wagombea 24 wakichukua fomu za kugombea.

Jna Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama Alexandrina Katabi, alisema kuwa waliochukua fomu na kuzirudisha katika  jimbo la Kahama ni wagombea 15, jimbo la Msalala waliochukua fomu  na kurudisha wako saba na jimbo la  Ushetu waliochukua fomu na kuzirejesha ni watia nia watatu.

Katabi alisema kuwa wagombea wote waliochukua fomu wamerudisha fomu zao kwa ajili ya kujiandaa na maandalizi ya  kujinadi kwa wananchi ili waweze kuwapima kabla ya  kufanya uchaguzi wa kura za maoni August 01 mwaka huu.

Alisema kuwa mgombea mmoja ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Shinyanga Khamis Mgeja amejiondoa dakika za mwisho kwa madai kuwa hawezi kuwania nafasi hiyo huku rafiki yake Jumanne Kishimba akiwa pia ni mmoja wanaoiwania.

Hata hivyo katibu huyo wa CCM wilaya ya Kahama alisema kuwa, wagombea wote watafanya mchakato kwa pamoja na kwamba cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa  wanazingatia kanuni na taratibu za Chama katika harakati zao za kuwani kuchaguliwa ili kupata nafasi za kugombea nafasi walizoomba.

Wagombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM walianza kuchukua fomu Julai  15 na zoezi  hilo kumalizika Julai 19 mwaka huu ambapo  aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kahama James Lembeli  hakujitokeza kuchukua fomu ya kutetea nafasi  yake  huku kukiwa na kitendawili kuwa huenda katimukia chama cha Upinzani.

Duru za kuaminika ni kwamba Lembeli atagombea nafasi hiyo kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa madai kuwa chama cha mapinduzi kimepoteza mwelekeo kutokana na kukumbatia Rushwa.

Juzi akizungumuza na wandishi wa habari  nje ya ofisi za chama cha mapinduzi, Lembeli alisema kuwa hawezi kuwa sehemu ya ufisadi na rushwa zilizojaa ndani ya chama cha mapinduzi na kueleza kuwa atafikiria ni chama gani atahamia.

No comments:

Powered by Blogger.