LIVE STREAM ADS

Header Ads

SAFARI YA KUMTAFUTA ATAKAE LIKOMBOA JIMBO LA NYAMAGANA NDANI YA CCM YAANZA.

Huku akiwa na Ushawishi mkubwa, aliekuwa Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Pichani) ni miongoni mwa Makada wanaoomba ridhaa ya kupata nafasi ya kugombea Ubunge Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza.
 Na:Binagi Media Group
Makada 20 wamechukua na kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya kuipeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM katika jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza.

Makada hao wamejitokeza huku ajenda kubwa ndani ya chama chao ikiwa ni kumpata mgombea atakaeipeperusha vyema bendera ya chama na hatimae kulitwaa jimbo la Nyamagana kutoka mikononi mwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kilichoshinda jimbo hilo kupitia kwa kada wake Ezekiel Wenje katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Leo Makada hao wameanza kuzunguka katika Kata zote za Wilaya ya Nyamagana kwa ajili ya kujinadi kwa wanachama, kila mmoja akiomba ridhaa ya kupitishwa na chama ili kugombea Jimboni Nyamagana.

Wakijinadi mbele ya wanaccm katika Kata za Mbugani na Mabatini, kila mmoja miongoni mwa watia nia hao alikuwa akijinasibu kuleta mabadiliko zaidi ya kimaendeleo kupitia sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya na miundombinu ikiwa atapata ridhaa ya kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Nyamagana katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Makada hao ni Fikiri Aviaz Said, Dr.Malesa Mangu, Taus Shaban Halili, Raphael Zakaria Shilatu, Revocatus Rubigili Kimbwekuuli, Robert Mgendi Masunya, Komanya Erick Kitwala, Starehe Morice Dea pamoja na Mwl.Usandara Warioba Mahende.

Wengine ni Dr.Tumain Robert Lusenga, Dr.Silinus Elias Nyanda, Joseph Matanga Kahungwa, Mariam Maftaa Makene, Dr.Barnabas Mbogo, Angela Benedicto Mwangoza, Evod Thomas Kawishe, Stanslaus Shing'ong'o Mabula, Dede Petro Bonivetura na anaehitimisha watia nia 20 jimboni Nyamagana ni Pendo Samwel.

Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda amesema kuwa chama hicho kitahakikisha kinamsimamisha mgombea ambae anakubalika na wananchi bila kuwepo upendeleo wa aina yoyote.
Huku akiwa na kundi kubwa la madereva daladala na wajasiriamali, Dede Petro nae ni miongoni mwa Makada wanaoomba ridhaa ya kugombea jimbo la Nyamagana.
Akiwa na Uzoefu wa Kutosha katika siasa, Raphael Shilatu ni mmoja wa watia nia jimbo la Nyamagana.
Akiwa na Uzoefu wa Kutosha katika siasa, Raphael Shilatu ni mmoja wa watia nia jimbo la Nyamagana.
Robert Masunya nae ni miongoni mwa watia nia jimbo la Nyamagana
Watia nia Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza
Watia nia Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza
Kushoto ni Jesca Mbogo ambae ni Mwenyekiti wa UWT Tawi la SAUT ambae pia amejitosa kuwania Ubunge Viti Maalumu akiwakilisha Kundi la Vijana Jimbo la Nyamagana (CCM) na kulia ni Kada wa Chama (CCM) Caroline Masanja ambae pia ni Mkufunzi UWT Mkoa wa Mwanza. Hakika palipo na mafanikio jua akina mama hawakosekani, sote twajua UWT SAUT ilivyo na nguvu hivi sasa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda akizungumza jambo hii leo wakati watia nia walipokuwa wakijinadi kwa wanachama katika Mkutano Kata ya Mbugani na Mabatini.
Wananzengo wakifuatilia mchakato.

No comments:

Powered by Blogger.