LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMANDA JOHN BUYAMBA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA.

Aliekuwa Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Misungwi John Buyamba (Kulia) akionyesha fomu ya kuwania kugombea Ubunge jimbo la Ilemela.
 Na:George GB Pazzo
Makada mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, wameendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho ili kugombea nafasi za uongozi kwa ngazi za Udiwani na Ubunge.

Zaidi ya Makada sita wa chama hicho tayari wamejitokeza na kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Ilemela, ambapo miongoni mwao  ni aliekuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM yaani UVCCM Wilaya ya Misungwi John Buyamba ambae jana alichukua fomu ya kugombea.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Buyamba ambae pia aliwahi kuwa ni Mjumbe wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, alisema kuwa akipata nafasi anayoiwania atahakikisha anashirikiana na wananchi kwa lengo la kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo mbiundomimbu, Afya pamoja na Elimu.

Katika ngazi ya Udiwani, pia mchakato wa Uchukuaji fomu umeendelea katika Wilaya ya Ilemela ambapo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Abdulrahman Khalfan Kange nae jana alijitokeza na kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika Kata hiyo na hivyo kufanya idadi ya waliochukua fomu kufikia makada watatu.

Baada ya kuchukua fomu, Kange ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mwanza, alibainisha kuwa akipata fursa ya kuwa diwani wa Kata ya Nyamanoro atajikita zaidi katika kuondoa kero mbalimbali zinazoikabili Kata hiyo ikiwemo kuboresha upatikanaji wa miundombinu ya maji pamoja na elimu.

Kwa pamoja Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi pamoja na Bahati Masoud Ramadhan ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro, waliwasihi watia nia wote waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea, kuzingatia katiba ya chama, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ikiwemo kuachana na siasa za kuchafuana wenyewe kwa wenyewe, kwani atakaebainika kukiuka taraibu hizo, jina lake halitaweza kupitishwa na vikao vya chama.


Fomu za kuwania udiwani na ubunge katika Chama cha Mapinduzi CCM zilianza kuchukuliwa Julai 15 na mwisho wa kurejesha fomu hizo unatarajiwa kuwa Julayi 19, mwaka huu majira ya saa kumi za alasiri hivyo watia nia wote wametakiwa kuzingatia muda uliopangwa.
Pongezi baada ya Kuchukua Fomu
John Buyamba akijaza fomu
John Buyamba (Kushoto) akipokea fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Ilemela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Achen Maulidi (Kulia).
Gharama za fomu zilikilipwa kwanza
John Buyamba akijaza fomu ya kugombea kuwania kugombea ubunge jimbo la Ilemela (CCM)
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi akizungumza na wanahabari.
Binagi Media Group Productions

No comments:

Powered by Blogger.