LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYEKITI WA UVCCM KATA YA NYAMANORO WILAYANI ILEMELA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA.

Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kushoto) jana akichukua fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan akimkabidhi fomu hiyo ambayo gharama yake ni shilingi elfu hamsini.
 Na:George GB Pazzo
Makada mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, wameendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho ili kugombea nafasi za uongozi kwa ngazi za Udiwani na Ubunge.

Zaidi ya Makada sita wa chama hicho tayari wamejitokeza na kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Ilemela, ambapo miongoni mwao  ni aliekuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM yaani UVCCM Wilaya ya Misungwi John Buyamba ambae jana alichukua fomu ya kugombea.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Buyamba ambae pia aliwahi kuwa ni Mjumbe wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, alisema kuwa akipata nafasi anayoiwania atahakikisha anashirikiana na wananchi kwa lengo la kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo mbiundomimbu, Afya pamoja na Elimu.

Katika ngazi ya Udiwani, pia mchakato wa Uchukuaji fomu umeendelea katika Wilaya ya Ilemela ambapo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Abdulrahman Khalfan Kange nae alijitokeza na kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika Kata hiyo na hivyo kufanya idadi ya waliochukua fomu kufikia makada watatu.

Baada ya kuchukua fomu, Kange ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mwanza, alibainisha kuwa akipata fursa ya kuwa diwani wa Kata ya Nyamanoro atajikita zaidi katika kuondoa kero mbalimbali zinazoikabili Kata hiyo ikiwemo kuboresha upatikanaji wa miundombinu ya maji pamoja na elimu.

Kwa pamoja Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi pamoja na Bahati Masoud Ramadhan ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro, waliwasihi watia nia wote waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea, kuzingatia katiba ya chama, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ikiwemo kuachana na siasa za kuchafuana wenyewe kwa wenyewe, kwani atakaebainika kukiuka taraibu hizo, jina lake halitaweza kupitishwa na vikao vya chama.

Fomu za kuwania udiwani na ubunge katika Chama cha Mapinduzi CCM zilianza kuchukuliwa Julai 15 na mwisho wa kurejesha fomu hizo unatarajiwa kuwa Julayi 19, mwaka huu majira ya saa kumi za alasiri hivyo watia nia wote wametakiwa kuzingatia muda uliopangwa.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kushoto) akilipa pesa kwa ajili ya gharama ya kuchukua fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan akipokea pesa hizo ambazo ni shilingi elfu hamsini. Aliekaa kushoto ni Khadija Iddy mkewe Kange.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Katika) akionyesha fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan na kushoto ni Khadija Iddy mkewe Kange.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) baada ya kuchukua fomu akiwa na mkewe Khadija Iddy (Kushoto).
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akiwa na mkewe Khadija Iddy (Kushoto) wakati wa kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akijiandikisha ili kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro ambapo kushoto ni mkewe Khadija Iddy.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akijiandikisha ili kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro ambapo kushoto ni mkewe Khadija Iddy.
Mbele ya Wanasa matukio, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Kulia) akijiandikisha ili kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata ya Nyamanoro ambapo kushoto ni mkewe Khadija Iddy.
Katibu wa CCM Kata ya Nyamanoro Bahati Masoud Ramadhan
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Abdulrahman Khalfan Kange (Wa tatu kushoto) akiwa pamoja na makada na viongozi wa CCM Kata ya Nyamanoro.
Binagi Media Group Productions

No comments:

Powered by Blogger.