LIVE STREAM ADS

Header Ads

KASI YA LOWASA KUINGIA MAGOGONI YAZIDI KUPAMBA MOTO. ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS. MAMIA WAJITOKEZA KUMSINDIKIZA KAMA KAWAIDA.

Binagi Media Group
Siku ya tatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akitokea Chama cha Mapinduzi CCM, aliekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Ngoyai Lowasa, leo amechukua Fomu ya Kugombea Urais.

Mamia ya Wananchi pamoja na makada wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, yamejitokeza katika kumsindikiza Lowasa wakati wa zoezi la Uchukuaji wa Fomu lililofanyika Makao Makuu ya Chadema Jijini Dar es salaam.

Lowasa amechukua fomu huku viongozi waliodaiwa kutokubaliana na maamuzi ya yeye kupokelewa chadema wakiwepo ambao ni pamoja na Katibu Mkuu Dk.Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika pamoja na Mwanasheria Mkuu Tundu Lisu.

Duru za kisiasa kutoka ndani ya vyama vinavyounda Ukawa zinaeleza kuwa Lowasa anatarajia kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu unaotarajia kufanyika Octoba 25 akiwakilisha Vyama vinavyounda Ukawa.

Hata kabla ya kampeni za wagombea kuanza rasmi, mchuano umeonekana kuwa mkali katika vijiwe mbalimbali na hata katika mitandao ya kijamii ambapo mijadala mikali ni kati ya Lowasa na Mgombea wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli.

No comments:

Powered by Blogger.