LIVE STREAM ADS

Header Ads

RUNINGA UPANDE WA DEREVA KATIKA DALADALA HII, NI HATARI KWA USALAMA WA ABIRIA NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA.

Habari za Wakati huu wapendwa wasomaji Wa Binagi Media Group. Ni matumaini yetu ya Kwamba mtandao huu unasomwa na watu mbalimbali wakiwemo Madereva, Abiria na hata maaskari wa Usalama barabarani. 

Kwa mantiki hiyo leo tunaweka pembeni mbwembe zetu za uandishi na kuungana live na mmoja wa wasomaji wetu ambae anatueleza moja ya tabia ambazo si nzuri zinayofanywa na baadhi ya madereva Jijini Mwanza na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria na baada ya hapo tutafute suluhisho juu ya tatizo hilo iwe ni kwa vitendo au ushauri.

Inaanzia hapa "Kuna daladala moja nimepanda leo ya kutoka Kishiri kuelekea Airport (Kisesa-Mecco-Airpot yenye nambari T 778 CLL). Ndani ya gari hiyo kuna Tv mbili, moja ni kubwa ambayo abiria wote tunaweza tizama na nyingine ni kadogo sana kapo pale mbele kwa dereva.

Kitu ambacho kimenifanya niwashirikishe wenzangu ni kwamba huyo dereva alikuwa anatizama kale katv kadogo huku anaendesha gari, ilifikia wakati kidogo aigonge gari ya mbele maana alikuwa busy anatizama tv.

Haikuishia hapo tulipofika maeneo ya ghana tena akafunga break ghafla kwa sababu ile ile.

Jamani kwa mazoea haya hv ajali zitapungua kweli? Abiria tumemwambia sana lakini hajatilia maanani.
Nimebahatika kupiga picha namba za gari ili tusaidiane kukOmesha matatizo haya". Anamaliza kusimulia.
Karibuni kwa ushauri na msaada zaidi...

No comments:

Powered by Blogger.