LIVE STREAM ADS

Header Ads

LEMBELI AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI JIMBO LA KAHAMA MJINI. SASA KUIPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA.

Na:Shaban Njia
Baada ya kujiunga na  Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, aliekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama James Daudi Lembeli kupitia CCM, ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CHADEMA kwa kupata kura 168 kati ya kura 262 za wajumbe wote waliopiga kura za kupata mgombea katika Jimbo la Kahama Mjini.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi kanda ya Serengeti Haile Sizza Tarai, alimtangaza James Lembeli kuwa mshindi ambapo ataipeperusha bendera ya chadema katika jimbo la kahama kwa kushirikiana na wajumbe na viongozi mbalimbali kuchupa ushindi.

"Kura zilizopigwa ni 262 na zilizoharibika ni tatu, ambapo Lembeli amepata kura 168 akifuatiwa na John Emmanuel Kipigu kura 45, Anold Peter Nshibo kura 17 pamoja na Emmanuel Mseza Madoshi kura 10". Alisema Tarai

Akizungumza baada ya matokeo kutangzwa, Lembeli alisema kuwa safari ya Chadema kwenda kuchukua majimbo yote matatu yaliyopo katika Wilaya ya Kahama imewadia hivyo CCM ijiandae kung'oka madarkani.

“Ndugu zangu wanachadema ushindi nilioupata unaashiria moja kwa moja tunakwenda kuchukua majimbo yote ya Kahama kwa kuwa chama chetu tunajamini sana na huwa hatushindwi kwa chochote kama tuliweza kushinda katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa". Alisema Lembeli.

Akizungumza kwa niamba ya watiania walioshindwa katika kinyanganyiro hicho, Katibu wa Chadema Mkoa wa shinyanga Zacharia Thomas Obad aliahidi kuwa chama hicho kitashirikiana na Lembeli kwau karibu ili kuhakikisha kwamba wanashinda jimbo la kahama mjini.

No comments:

Powered by Blogger.