LIVE STREAM ADS

Header Ads

KIJANA PETER ANDREW (19) MWENYE KIPAJI CHA AJABU ATUNUKIWA CHETI CHA UTAMBUZI NA BSS 2015.

Mbali na kusaka Wenye vipaji vya uimbaji, Mwaka huu pia Shindano la Bongo Star Search limetambua watu wenye vipaji vya aina mbalimbali ambavyo vikiendelezwa vinaweza kuleta mapinduzi makubwa hapa nchini.
Na:George GB Pazzo
Katika Usaili wa BSS 2015 uliofanyika Mkoani Mwanza jumamosi na Jumapili iliyopita, Kijana PETER ANDREW (miaka 19 (Pichani) kutoka Mkoani Geita ametunukiwa cheti cha utambuzi wa Kipaji chake cha kipekee baada ya kufanikiwa kutengeneza zana za kifizikia za aina mbalimbali licha ya kwamba kijana huyu ambae ni mhitimu wa kidato cha nne alikuwa ni mwanafunzi wa masomo ya sanaa na si Sayansi.

Kijana huyu amefanikiwa kutengeneza Mtambo wa kuhisi sauti ambao una uwezo wa kuwasha taa kwa MFUMO WA SAUTI bila Switch kuhitajika.

Ukitamka WAKA/ON mtambo huo huwasha taa ya Umeme na Ukitamka ZIMA/OFF mtambo huo pia huzima taa hiyo. Lakini pia hata ukiwa Mkoa mwingine unaweza kutumia Mtambo huo kuwasha au kuzima taa iliyo nyumbani kwako katika Mkoa tofauti kwa kupiga nambari ya simu iliyounganisha na Mtambo huo.

Mbali na hayo, Kijana huyo ametengeneza SCREEN TOUCH kwa kutumia kioo cha Kujiangalizia pamoja na Radio ambayo ina uwezo wa kubadili masafa yake kwa kutumia kivuli cha mkono wako ukiwa unaitumia. 

Hakuna haja ya kubonyeza sehemu yoyote bali unaelekeza tu kidole chako na masafa yanabadilika. Mfano kama ulikuwa unasikiliza masafa ya Radio Metro Fm unaweza kuyabadili bila kuigusa radio hiyo na ukahamia katika Masafa ya Binagi Radio kwa kuelekeza tu mkono wako hewani kwenda kulia au kushoto na masafa yakabadilika.

"Nina uwezo wa kutengeneza vitu vingi sana lakini ndo hivyo tena bado natumia vifaa duni lakini nikipata nafasi ya kwenda kusoma zaidi nje ya nchi nitaweza kutengeneza vitu na vikubwa zaidi ya hivi. Niliwahi kutengeneza hata Calculata sema tu ikawa inahitaji maboresho zaidi maana hesabu zake zilikuwa zikiishia 99 tu lakini nina uwezo wa kutengeza yenye uwezo zaidi ya hiyo". Anasema Andrew na kuongeza kuwa;

"Tanzania nimekosa chuo kinachoweza kunipokea ili nikasome zaidi maana sekondari sikusoma masomo ya sayansi hivyo nakosa sifa ya kujiendeleza kielimu hapa nchini kwa vyuo ambavyo naweza kusomea masuala yangu haya vinapokewa wanafunzi waliosoma phisycs na ndiyo maana nahitaji msaada zaidi ili nikasome nje ya nchi ambapo mwanafunzi anapata fursa ya kusoma kulingana na kipaji chake".Anabainisha Endrew.

Kutokana na hayo, Bongo Star Search 2015 ilimtunuku Peter Andrew cheti cha utambuzi wa kipaji chake, akiwakilisha Mkoa wa Mwanza hivyo USIKOSE KUFUATILIA BSS 2015 KUPITIA CLOUDS TV & STAR TV KUANZIA JULAI 19,2015 SIKU YA JUMAPILI ILI KUJIONEA ZAIDI.
Peter Andrew akirekebisha mtambo wake.
Peter Andrew akifunga mtambo wake
BINAGI MEDIA GROUP, KIPAJI HIKI KISIACHWE KIPOTEE BURE.
Picha zote na MX @BSS 2015
Tazama picha za Usaili BSS 2015 Mwanza HAPA

No comments:

Powered by Blogger.