LIVE STREAM ADS

Header Ads

SUMU: VIJANA MHONZE WALIOPO ILEMELA MKOANI MWANZA WAPATA HASARA YA TAKRIBANI MILIONI TANO.

Hawa ni baadhi ya Samaki waliokufa katika bwawa la Samaki la Kikundi cha Vijana Mhonze Kilichopo Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza baada ya Watu wasiojulikana kusadikika kuwa jana jumapili Julai 05, 2015 walimwaga sumu katika bwawa hilo na hivyo kusababisha samaki waliokuwa katika bwawa hilo kufa.
Na:George GB Pazzo
Hadi sasa inakadiliwa kuwa uharibifu huo umesababisha hasara ya takribani shilingi milioni tano. Mradi huo ulianza mwaka jana mwezi Novemba ukiwa na samaki Mia Tano katika mabwawa mawili na tayari vijana hao walikuwa wameanza mavuno.
Hawa ni baadhi ya wanakikundi cha Vijana Mhonze ambapo kutoka kushoto ni Katibu wa Kikundi Nelson Jackson, Masaga Budeba, Frank Laurent, Alfred Haroon pamoja na Alex Amos. 
Kikundi hicho kina wanachama 20.
Ilikuwa ni Masikitiko makubwa kwa kikundi hiki cha Vijana Mhonze
Mradi huu wa Ufugaji wa Samaki wa Vijana Mhonze ulianzishwa kwa usimamizi wa Shirika la Maendeleo ya Jamii na Kujengeana Uwezo la TAHEA lililopo Nyegezi Jijini Mwanza tangu mwezi Novemba mwaka jana ambapo takribani samaki 500 walipandikizwa katika Mabwawa mawili.
Afisa Miradi kutoka Shirika la TAHEA Mussa Masongo akijionea uharibifu uliotekea katika bwawa la samaki la Vijana Mhonze Wilayani Ilemela baada ya watu wasiojulikana kusadikiwa kumwaga sumu katika bwawa hilo na kusababisha samaki waliokuwemo kufa.
Kikundi hicho cha Vijana Mhonze kinamiliki Mabwawa mawili na bwawa moja ndilo limeathirika zaidi kutokana na sumu iliyomwaga na watu wasiojulikana. Mabwawa hayo yamezungushiwa Fensi lakini waharifu hao waliikata kama inavyoonekana katika picha.
Katibu wa Kikundi cha Vijana Mhonze Nelson Jackson (Katikati) akieleza juu ya Mkasa uliowasibu
Kushoto ni Evarist Chikaga ambae ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugunda ulipo Mradi wa Ufugaji Samaki wa Vijana Mhonze akielezea juu ya tukio la bwawa la wanakikundi hicho kuwekewa sumu na kusababisha samaki waliokuwemo kufa.
Kulia ni Alpha Ernest Benge ambae ni Afisa Uvuvi Msaidizi Manispaa ya Ilemela akifafanua kwamba; sampuli ya maji na samaki waliokufa itachukuliwa na kupelekwa maabara ili kupata uhakika wa sumu iliyomwagwa katika bwawa la samaki linalomilikiwa na kikundi cha Vijana Mhonze na kusababisha samaki waliokuwemo Kufa.
Kushoto ni Faraji Faustine Paragha ambae ni Mhamasishaji Vijana Kutoka Shirika la Miradi ya Maendeleo na Kujengeana Uwezo la TAHEA lililopo Nyegezi Jijini Mwanza akizungumza na wanahabari juu ya mradi wa ufugaji Samaki wa Vijana Mhonze ambao shirika hilo lilishiriki ipasavyo wakati unaanzishwa Mwezi Novemba mwaka jana.
Kushoto ni Alpha Ernest Benge ambae ni Afisa Uvuvi Msaidizi Manispaa ya Ilemela akichukua samaki waliokufa kwa kile kinachosadikika kuwa ni sumu kwa ajili ya kupelekwa maabara ya uvuvi kwa uchunguzi zaidi.Kulia ni Katibu wa Kikundi cha Vijana Mhonze Nelson Jackson.
Alpha Ernest Benge ambae ni Afisa Uvuvi Msaidizi Manispaa ya Ilemela akichukua maji ya bwawa ambalo inasemekana limemwagwa sumu kwa ajili ya kupelekwa maabara ya uvuvi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Geti la kuingilia yalipo Mabwawa mawili ya Ufugaji samaki yanayomilikiwa na Kikundi cha Vijana Mhonze
Mabwawa ya Ufugaji Samaki Mhonze yaliyopo Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Nelson Jackson ambae ni Katibu wa Kikundi cha Ufugaji Samaki Vijana Mhonze kilichopo Ilemela Mkoani Mwanza akiwa katika ofisini ya kikundi hicho
Soma bango kwa Umakini
Nikiripoti kutoka Mhonze Kata ya Bugogwa, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza huku nikiwa na hasira kama Simba aliejeruhiwa baada ya Watu wachache wasiopenda maendeleo ya Wenzao kusadikika kuwa wamemwaga sumu katika Bwawa la Samaki linalomilikiwa na Kikundi cha Vijana Mhonze na kusababisha Samaki waliokuwemo Kufa, Mimi ni GB Pazzo wa Radio Metro na Binagi Media Group.

No comments:

Powered by Blogger.