LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA SOKA YA MWAMANYILI YAIBUKA BINGWA WA MASHINDANO YA BULUBA SUPER CUP MKOANI SIMIYU.

(Picha haina uhusiano na habari)
Na:Oscar Mihayo
Mashindano ya soka ya Buluba Super Cup yamefikia tamati hapo kwa timu ya Mwamanyili kuibuka bingwa wa mashindano hayo kwa kuilaza timu ya Nyashimo kwa penati 4-3 katika uwanja wa shule ya msingi Nyashimo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mpambano huo ambao ulipigwa juzi jumapili ulikuwa na upinzani mkali ambapo uliingia hatua ya matuta baada ya dakika za kawaida za mchezo kumalizika kwa suruhu ya bao 1-1 ambapo mfungaji wa bao la mwamanyili alikuwa ni Frank Magungwa na bao la Nyashimo likifungwa na Hassan Abdallah.

Mfadhili wa mashindano hayo Buluba Mabelele alikabidhiwa Ng’ombe wawili wenye thamani shilingi  (800,000) kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili alipewa ng’ombe mmoja mwenye thamani ya shilingi (400,000) na mshindi wa tatu akapatiwa mbuzi wa tatu wenye thamani ya shilingi (180,000).

Mfadhili huyo alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji pamoja na kupata timu ya kushiriki Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa Mkoa huo.

Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo Yusuph  Budodi aliongeza kuwa kabla ya mechi ya fainali kuanza ilitanguliwa na mchezo wa timu ya vijana ya nasarmido na Kalemela ampapo kwa pamoja walipewa seti moja ya jezi na Daftari 100 kutoka kwa mfadhili wa mashindano hayo.

Budodi aliongeza kuwa vikundi vya ushangiliaji kwa wakina mama  kwa ngoma za asili  navyo vilikuwa vikichuana ambapo kikundi cha  mwamanyili kilishinda na kujinyakulia mbuzi wanyama wa tatu.

Aidha aliongeza kuwa mashindano hayo ya tatu tangu kuanzishwa kwake ni endelevo na kila mwaka yamekuwa yakiingia na sura tofauti huku akisema mwakani yataboreshwa zaidi huku akizitaka timu shiriki kujiandaa vya kutosha mapema.

No comments:

Powered by Blogger.