LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUMEKUCHA BONGO STAR SEARCH 2015 JIJINI MWANZA. WASANII KUTOKA MIKOA JIRANI WAIBUKA WA WINGI.

Hawa ni baadhi ya Wasanii waliojitokeza katika Usaili wa kusaka Vipaji vya Wanamuziki la katika Shindano la BONGO STAR SEARCH 2015 ikiwa huu ni Msimu wa Nane tangu Shindano hilo Kuanzishwa hapa nchini. 
Picha na Vesterjtz
Wasanii chipukizi kutoka Mkoani Mwanza pamoja na Mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa wamejitokeza kwa wingi katika Usaili wa kusaka Vipaji vya kuimba katika Shindano la BONGO STAR SEARCH 2015.

Usaili huo unafanyika La Kairo Hotel Jijini Mwanza ambapo kila mmoja anasema kuwa amejiandaa vyema ili kupata nafasi ya kushiriki Shindano hilo kwa lengo la kuibuka Star mwaka huu na hivyo kujinyakulia Kitita cha fedha kilichotengwa mwaka huu.

Wadhamini wakuu wa Shindano hilo la BONGO STAR SEARCH 2015 ambalo litakuwa likionyeshwa katika Runinga za Star Tv na Clouds Tv ni SALAMA CONDOM "KUWA ORIGINAL, CHAGUA ORIGINAL"

Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano hilo la Bongo Star Search, Rita Paulsen anasema kuwa mwaka huu shindano hilo limeboreshwa zaidi ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Mamilioni ya fedha huku washindi watakaoingia tano bora wakiwekwa chini ya Menejimenti ya Kundi la Tip Top Conection.

Mkoani Mwanza usaili umeanza hii leo Juli nne hadi kesho Julai Tano katika ukumbi wa La Kairo Hotel ambapo zaidi ya wasanii 300 wamejitokeza katika usaili, July 11 hadi Julai 12 itakuwa ni Mkoani Arusha katika ukumbi wa Triple A Hotel, July 18 hadi Julai 19 usaili utafanyika Mkoani Mbeya katika ukumbi wa Club Vibes ambapo hitimisho la usaili litafanyika Jijini wa Dar es Salaam Julai 24 hadi Julai 26 mwaka huu.
Tayari kabisa kwa ajili ya Shindano la Bongo Star Search 2015
MWANZA, HAPA NDIPO BONGO STAR SEARCH INAANZIA
Vipaji vikiendelea kupokelewa.
Usaili ukiendelea kusahiliwa
Hapa kazi tu
Vipaji Original
Bongo Star Search 2015 ni Nomaaaaaaaa
Ze Nyomi zikisubiria kuitwa ili kuonyesha Uhodari wa Kuimba baada ya kupata namba ya ushiriki.
ANAITWA GODFREY BINAGI...HAPO AWALI HAIKUJULIKANA KM ANA KIPAJI CHA UIMBAJI NA HATA FAMILIA YAKE PIA HILO HAIKULIJUA.
BAADA YA KUHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA HUU, AMEAMUA KUJITOSA RASMI KTK MUZIKI.
HAPA YUPO KTK USAILI WA BONGO STAR SEARCH JIJINI MWANZA KTK HOTEL YA LAKAIRO....
YETU MACHO ILI TUJUE KAMA KWELI ANA KIPAJI NA TUMWOMBEE KILA LA KHERI ILI AFIKIE NDOTO ZAKE.BONGO STAR SEARCH 2015 KUWA ORIGINAL...SPONSORED BY SALAMA CONDOM.
Wanahabari ambapo kutoka kushoto ni Jonson @gazeti la Champion, kulia waliokaa ni DullahTza @Millardayo.com, katikati ni Vesterjtz @Afya Radio & Binagi Media Group na Kushoto ukutani ni GB Pazzo @Radio Metro & C.E.O Binagi Media Group.
Wanahabari ambapo kutoka kushoto ni Rodrick Ngowi @gazeti la Mtanzania, kulia waliokaa ni DullahTza @Millardayo.com, katikati ni Vesterjtz @Afya Radio & Binagi Media Group na Kushoto ukutani ni GB Pazzo @Radio Metro & C.E.O Binagi Media Group.

No comments:

Powered by Blogger.