LIVE STREAM ADS

Header Ads

MMOJA AUAWA NA POLISI JIJINI MWANZA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI HUKU WAWILI WAKITOKOMEA.

Alieuawa katika tukio la Ujambazi Jijini Mwanza jana
(Picha na Mdau-Binagi Media Group, Whatspp namba yetu ni 0757 43 26 94).
Na:George GB Pazzo
Mtu mmoja aliesadikiwa kuwa ni Jambazi ameuawa Jijini Mwanza na Jeshi la Polisi huku wenzake wawili wakifanikiwa kutokomea kusikojulikana, baada ya kurushiana risasi na Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana katika eneo la Nyegezi baada ya polisi kuwashtukia watu watatu waliokuwa katika pikipiki kuwa ni waharifu na kutaka kuwasimamisha, lakini ghafla watu hao walianza kujihami kwa risasi.

"Huko katika eneo la Nyegezi, polisi waliishtukia pikipiki moja iliyokuwa imewabeba watu watatu waliosadikiwa kuwa ni majambazi na baada ya kuishukia pikipiki hiyo ghafla mmoja wa watu hao alitoa bunduki na kuanza kulishambulia gari la polisi lakini kwa ujasiri mkubwa askari walisimama kidete na kupambana nae na kumdondosha chini huku wenzake wawili wakifanikiwa kutoroka". Alisema Kamanda Mkumbo.

No comments:

Powered by Blogger.