LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKOA WA DAR ES SALAAMU WAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MASHINDANO YA UMITASHUMITA TAIFA.

Na:Oscar Mihayo
Mkoa wa Dar es Salaam umeibuka bingwa wa jumla kwa alama 36 katika mashindano ya  Umoja wa michezo na Taaluma kwa shule za msingi UMITASHUMITA kitaifa, yaliyomalizika hii leo katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mkoa wa Mbeya kwa alama 36 huku nafasi ya tatu ikibakia kwa wenyeji Mkoa mwenyeji Mwanza kwa kupata alama 28.

Akifunga mashindano hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi kitengo cha Elimu Majaliwa Kassimu ambaye alikuwa Mgeni rasmi, alizitaka halmashauri zote nchini kupitia baraza la madiwani kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia kuinua Michezo.

“Ili tufanikishe kwenye sekta hii muhimu  hatuna budi kushirikisha wadau wapenda michezo zikiwemo taasisi binafsi ili kujipatia fedha za uendeshaji wa michezo hii ambayo ni muhimu sana kwa taifa letu kwa kuibua vipaji na kuwajenga vizuri watoto kupitia sekta hii ya michezo’’ alisema Kassimu.

Kassimu aliwataka  wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya viwanja vya michezo na kuviandaa kwa ubora zaidi ikiwa ni pamoja na kuviwekea ulinzi wa kutosha ili vitumike kwa ajiri ya michezo pekee.

Aidha aliitaka jamii yenye watoto wenye Mahitaji maalumu kama walemavu wa ngozi, wasio sikia na wasioona kuwatoa kwa ajili kushiriki katika mashindano hayo kwani serikali ameamua kuwapatia kipaumbele kwa kutambua umuhimu wao kama walivyo watoto wengine.

Alisema kuwa michezo hii itakuwa endelevu na kuhaidi mwakani kuirudisha Mwanza  baada ya kujiridhisha na usalama wa kutosha ikiwa ni pamoja ubora wa viwanja na mandhali nzima ya Jiji la Mwanza ambapo ameiomba sekretalieti ya mashindano hayo kujiandaa vyema zaidi ili mashindano hayo yafanyike kwa ufasaha zaidi.

Kwa upande wake Mratibu mkuu wa mashindano hayo ua UMITASHUMITA kutoka Tamisemi Mohamed Kiganja aliwahimiza wazazi kuwa na desturi ya kujitokeza kuwashangilia watoto wao katika Mashindano hayo kwani kufanya hivyo ni kuongeza hamasa ya wao kufanya vizuri huku akiwataka kuachana na dhana potofu ya kuwazuia watoto wao kushirika michezo wakidhania ni upotevu wa muda. 

Aliongeza kuwa kwa sasa wanajiandaa kuwaendeleza vijana waliochaguliwa katika Mashindano hayo kwa kushiriki mashindani ya Africa mashariki.

No comments:

Powered by Blogger.