MAGUFULI AWAAHIDI NEEMA WANAKAHAMA.
Na:Shaban Njia
Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr.John Pombe Magufuli, ameendeleza kauli yake ya kudai kuwa hatawaangusha Watanzania pindi atakachaguliwa katika wadhifa huo Oktoba 25 mwaka huu huku akidai kwamba wakati utakapofika atakuwa na ahadi yenye neema kwa wakazi wa Wilaya ya Kahama.
Akizungumuza jana na wanachama wa Chama cha Mapinduzi, waliojitokeza katika ofisi za chama hicho wilaya ya Kahama,Dr.Magufuli alisema amepita kujitambulisha kwa wakazi wa wilaya ya Kahama akitokea mkoani Geita navkubainisha kuwa changamoto za wilaya ya Kahama anazifahamu hivyo wakati utakapofika atazianisha kuzitatua.
Alisema anatambua ukubwa wa mji wa Kahama na kwamba kasi ya maendeleo iliyopo katika Wilaya hiyo hailingani na hadhi yake , na kuwahakikishia kuwa kulingana na ilani ya chama chake wilaya hiyo itafikia hadhi stahiki kulinagana na ukuaji wake.
Alisema kuwa ipo mikoa mingi hapa nchini ilipewa hadhi ya kuwa mikoa lakini haijafikia idadi ya watu waliopo wilayani Kahama,jambo analofikiria atakapofika katika Kampeni atahakikisha anasimamia ilani ya chama cha mapinduzi CCM ili wilaya ya Kahama ipate stahiki yake ya kuwa Mkoa kulingana na kasi ya maendeleo yake na wingi wawatu.
Alisema atahakikisha anadumisha msingi imara wa upendo pasipo kujali tofauti za kiitikadi za vyama,dini ama kabila hatua itakayosaidia kuondoa matabaka ya baadhi ya Watanzania kuona miongoni mwao ni bora kiasi cha kufikia kuogopwa na kutoshirikiana na wengine jambo ambalo ni kukiuka mila na desturi za Kitanzania.