LIVE STREAM ADS

Header Ads

MNEC NA MKURUGENZI WA NYANZA BOTTLING, CHRISTOPHER GACHUMA AFUTURISHA JIJI MWANZA.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM, MNEC Mh.Christopher Mwita Gachuma wakichukua Futari/chakula. 
Kwa Upande wa Wanaume, Hafla hiyo ilifanyika Katika Ukumbi wa Roof Top ndani ya New Mwanza Hotel jana Jumamosi Julai 04, 2015 huku kwa upande wa Wanawake ikifanyika katika Ukumbi wa Kipepeo hotelini hapo.

Wananchi bila kujali itikadi za kidini, Viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, taasisi na Vyama mbalimbali walihudhuria katika Iftar hiyo ya Ramadhan ambayo huandaliwa kila mwaka na MNEC Gachuma. 
Na:George GB Pazzo
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae katika hotuba yake aliwasihi Viongozi wa dini kusaidia katika kudumisha amani ya Mkoa wa Mwanza isitoweke hususani katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu ambapo alionya Kuwa Serikali imejizatiti katika kuhakikisha inailinda Amani iliyopo.

Alionya juu ya vikundi vya kisiasa vinavyoundwa mitaani/msituni kwa lengo la kulinda kura wakati wa uchaguzi ambapo alisema kuwa Serikali iko macho na haitaviacha vikundi hivyo kuvuruga amani iliyopo kwa kufanya fujo kwa kisingizio cha kulinda kura.

Aidha alizungumzia zoezi la Uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo alibainisha kuwa zoezi hilo linaendelea vyema katika Mkoa wa Mwanza na hadi kufikia sasa limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 Mkoani Mwanza.
Ni muda wa Chakula/ Futuru
MNEC Christopher Mwita Gachuma ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyanza Bottling (Wa kwanza Kulia) akiwa pamoja na wageni waalikwa wakipata chakula/Futuru.
Futuru ikiendelea
MNEC Christopher Mwiita Gachuma akiwa (Kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia).
Wa kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiwa na Waalikwa wengine wakipata Futuru/ Chakula
Futuru/Chakula
Futuru Time
Futuru
Baada ya Futuru ukawadia wasaa wa hotuba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (hayuko pichani) na hapa waalikwa wakifuatilia neno kwa ukaribu zaidi.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hida (Kulia) akiwa na Waalikwa wengine
Futuru/ Chakula time
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mwauasa Antony Sanga (Kushoto) na Waalikwa wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Kulia) akitoa hotuba yake baada ya Futuru ambapo zaidi alisisitiza juu ya Viongozi wa dini kusaidia katika kudumisha amani ya Mkoa wa Mwanza isitoweke hususani katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu ambapo alisema Kuwa Serikali imejizatiti katika kuilinda Amani iliyopo.
 Alionya juu ya vikundi ambavyo vinaundwa mitaani kwa ajili ya kulinda kura wakati wa uchaguzi kwa kusema kuwa Serikali iko macho na haitaviacha vikundi hivyo viivuruge amani iliyopo.

Aidha alizungumzia zoezi la Uandikishaji wananchi katika daftari la wapiga kura ambapo alisema kuwa linaendelea vyema katika Mkoa wa Mwanza na hadi kufikia sasa limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 Mkoani Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza ambapo alisema kuwa suala la Gachuma kuwakutanisha waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wasio waumini wa dini hiyo katika Futuru ni jambo jema na la kuigwa katika jamii.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Sheikh Mohamed Salum Bala akitoa nasaha zake
Katibu wa Jukwaa la Kuendeleza Quruan nchini Tanzani Sheikh Hassan Kabeke
Viongozi mbalimbali wa Kisiasa Mkoani Mwanza
MNEC Gachuma (Kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Mtaturu pamoja na Mmiliki wa Gazeti la Mzawa lililopo Mkoani Mwanz wakibadilishana Mawazo baada ya Futari.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana Hussein Kim (Kulia).
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kushoto) akiwa pamoja na Dr.Tonny @Radio Metro baada ya Futari.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Kushoto) akiwa na GB Pazzo (kulia) baada ya Futari.
GB Pazzo (Kushoto) akiwa pamoja na Mpiga picha wa Chanel Ten Mwanza Hussein Mtanda (Kulia).
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (katikati) akiwa na waalikwa wengine baada ya Futari.
Furaha na tabasamu tele baada ya Futari
Baada ya Futari
Baada ya Futuru
Kumbukumbu katika picha baada ya Futuru
Kumbukumbu katika Picha baada ya Futuru
Baada ya Futuru ilifuata Kumbukumbu katika Picha
Tazama picha za FUTURU ya Mwaka jana HAPA

No comments:

Powered by Blogger.