LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASHIRIKI MKOANI MWANZA WAPANIA KUSHINDA TAJI LA BONGO STAR SEARCH 2015.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen a.k.a Madame Rita, katika Judge Master J na Kulia ni Jugde Salama Jabiri.
Picha na Robert Kasamwa na Vesterjtz
Washiriki wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uimbaji la Bongo Star Search 2015 Mkoani Mwanza wameeleza kuwa watahakikisha kuwa wanafanya kila linalowezekana ili mshindi wa taji la shindano hilo atoke Mwanza.

Wakizungumza jana na Binagi Media Group katika Usaili unaofanyika Lakairo Hotel, baadhi ya washiriki waliojitokeza katika usaili huo walisema kuwa mwaka huu wamepania kuhakikisha kuwa taji la Bongo Star Search linadondokea Mkoani Mwanza ili kuupa tena hadhi kimuziki Mkoa huu.

"Mwaka huu tena washiriki kutoka Mkoani Mwanza tumejipanga vyema na lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunatoa Mshindi katika Shindano hili la Bongo Star Search kama ilivyokuwa mwaka miaka iliyopita". Walisema washiriki hao.

Washindi waliowahi kupitia kituo cha Mkoa wa Mwanza katika Shindano hilo la Bongo Star Search na Kuibuka mabingwa ni Pascal Cassim (2009), Haji Ramadhan (2011), Emmanuel Msuya (2013) pamoja na Kala Jeremiah ambae alikuwa mshindi wa pili mwaka 2007 wakati shindano hilo linaanza.

Wadhamini wakuu wa Shindano hilo la Bongo Star Search 2015 ambalo litakuwa likionyeshwa katika Runinga za Star Tv na Clouds Tv ni SALAMA CONDOM "KUWA ORIGINAL, CHAGUA ORIGINAL" ambapo kauli mbiu ni Kuwa Original, Jukwaa ni Lako.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano hilo la Bongo Star Search, Rita Paulsen anasema kuwa mwaka huu shindano hilo limeboreshwa zaidi ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Mamilioni ya fedha huku washindi watakaoingia tano bora wakiwekwa chini ya Menejimenti ya Kundi la Tip Top Conection.

Mkoani Mwanza usaili umeanza hii leo Juli nne hadi kesho Julai Tano katika ukumbi wa La Kairo Hotel ambapo zaidi ya wasanii 300 wamejitokeza katika usaili, July 11 hadi Julai 12 itakuwa ni Mkoani Arusha katika ukumbi wa Triple A Hotel, July 18 hadi Julai 19 usaili utafanyika Mkoani Mbeya katika ukumbi wa Club Vibes ambapo hitimisho la usaili litafanyika Jijini wa Dar es Salaam Julai 24 hadi Julai 26 mwaka huu.
Wasanii waliofika katika Usaili Mwanza
Jamaa wako tayari kuonyesha Uimbaji wao
The Wasanii katika Usaili Mkoani Mwanza.
Usaili Unaendelea
Katika Usaili Mkoani Mwanza
Timu ya Bongo Star Search 2015
Katika Usaiili
Fresh B a.k.a katika Usaili wa Bongo Star Search 2015
Wanahabari ambapo kulia waliokaa ni DullahTza @Millardayo.com, katikati ni Vesterjtz @Afya Radio & Binagi Media Group na Kushoto ukutani ni GB Pazzo @Radio Metro & C.E.O Binagi Media Group.

Tazama picha za Usaili HAPA

No comments:

Powered by Blogger.