LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAADVENTISTA WASABATO WAMCHAGUA TED WILSON KUWA KIONGOZI WAO MKUU DUNIANI MHULA WA PILI.

Washiriki wa Mkutano wa Uchaguzi wa Kumpata Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato duniani uliofanyika San Antanio Taxas nchini Marekani Julai 03, 2015 wakifuatilia mkutano huo kwa umakini kabisa.
Mkutano huo ulimchagua kwa mara ya pili TED WILSON kuwa Kiongozi Mkuu wa kanisa la Waadventista Wasabato duniani ambapo atalitumikia kanisa hilo katika awamu nyingine ijayo ya miaka mitano.
Na:Waitara Meng'anyi
Huyu ndiye Ted Wilson ambae alichaguliwa kwa asilimia 90 ya wapiga kura 1,900 waliomchagua Kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato duniani katika Uchaguzi uliofanyika Julai 03, 2015 huko San Antnio Taxas nchini Marekani. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Morning Star Radio walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Tanzania Adventister Internet Network TAiN 2015 wakiwa katika picha ya pamoja.

Kutoka Kushoto ni Eng.Daud Nyamajeje, anaefuata ni Abell Kinyongo (Arusha), anafuatia Prince Emmanuel (Dar), anaefuata ni Manase Rusaka na wa mwisho ni Waitara Meng'anyi (Tarime).

Mkutano Mkuu wa TAiN uliofanyika Jijini Arusha ulifanyika June 22 hadi June 24 Mwaka huu ukiwa na Kauli mbiu isemayo "Ubunifu Zaidi" ambapo uliwahusisha Watalaamu wa Mawasiliano na Waandishi wa Habari kutoka kanisa la Waadventista Wasabato kote nchini.
Washiri wa Mkutano Mkuu wa TAiN 2015 uliofanyika Jijini Arusha June 22 hadi June 24 Mwaka huu, wakiwa katika Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya Kumaliza Mkutano kwa Mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.