LIVE STREAM ADS

Header Ads

USAILI WA BSS 2015 MKOANI MWANZA WAKAMILIKA. KIVUTIO KILIKUWA KWA HUYU BIBI KUTOKA TABORA.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen a.k.a Madame Rita (katikati)akimpa mkono wa pongezi bibi kutoka Mkoani Tabora aliefika Jijini Mwanza katika Usaili wa Bongo Star Search (BSS 2015).

Bibi hakukatishwa tamaa kwani alijitahidi lakini pia alikuwa mshiriki mwenye umri mkubwa kuliko wote na hivyo kuonekana kivutio katika usaili huo.

Umri wake ni dhahiri shahiri kwamba asingeweza kuendana na kasi ya damu changa zilizojitokeza katika usaili huo hivyo ilibidi aambiwe jaribu tena mwakani.
Kushoto ni Judge Master J.
USIKOSE KUFUATILIA BSS 2015 KUPITIA CLOUDS TV & STAR TV KUANZIA JULAI 19,2015 SIKU YA JUMAPILI ambapo pia utawajua wawakilishi sita Kutoka Mkoani Mwanza.
Picha na MX @BSS
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen a.k.a Madame Rita, katika Judge Master J na Kulia ni Jugde Salama Jabiri.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmack Production inayoandaa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen a.k.a Madame Rita na kulia ni Judge Master J.
Mkoani Mwanza usaili ulifanyika juzi jumamosi Juli nne hadi jana jumapili Julai Tano katika ukumbi wa La Kairo Hotel ambapo baada ya usaili wa BSS 2015 unatarajia kuendelea katika Mikoa mingine.

July 11 hadi Julai 12 itakuwa ni Mkoani Arusha katika ukumbi wa Triple A Hotel, July 18 hadi Julai 19 usaili utafanyika Mkoani Mbeya katika ukumbi wa Club Vibes ambapo hitimisho la usaili litafanyika Jijini wa Dar es Salaam Julai 24 hadi Julai 26 mwaka huu.
TAZAMA PICHA ZA USAILI BSS 2015 MWANZA
Wadhamini wakuu wa Shindano hilo la Bongo Star Search 2015 ambalo litakuwa likionyeshwa katika Runinga za Star Tv na Clouds Tv ni SALAMA CONDOM "KUWA ORIGINAL, CHAGUA ORIGINAL" ambapo kauli mbiu ni Kuwa Original, Jukwaa ni Lako.

USIKOSE KUFUATILIA BSS 2015 KUPITIA CLOUDS TV & STAR TV KUANZIA JULAI 19,2015 SIKU YA JUMAPILI ambapo pia utawajua wawakilishi sita kutoka Mkoani Mwanza.
Kusoma walichokisema Washiriki wa BSS Mwanza bonyeza HAPA
Kuona Picha za Usaili wa BSS 2015 siku ya Kwanza bonyeza HAPA

No comments:

Powered by Blogger.