LIVE STREAM ADS

Header Ads

MULAGA SANGARA WAIBUKA MABINGWA WA MICHUANO YA HILANE WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA.

(Picha haihusiani na Habari)
Na:Oscar Mihayo
Michuano ya kombe la Hilane iliyokuwa ikitimua vumbi Sengerema Mkoani Mwanza, juzi imefikia tamati ambapi timu ya Mulaga Sangara FC iliibuka bingwa kwa kujinyakulia kombe pamoja na kitita cha shilingi Milioni Moja na Laki tano (1,500,000) baada ya kuichapa timu ya Mpogomi Star mabao 4-2 kwa mikwaju ya penati kufuatia dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mchezo huo ulikuwa wa upinzani mkali kwani timu zote mbili zilijiandaa vya kutosha huku mashabiki wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuushuhudia.

Timu ya Mpogomi Star iliibuka mshindi wa pili na kuzawadiwa kiasi cha Tsh.Milioni moja (1,000,000) na mshindi wa tatu Stand FC kupokea kitita cha shilingi Laki tano (500,000) mshindi wa nne Nyitundu FC akijipatia shilingi Laki Moja (100,000).

Katika mashindano hayo, mchezaji Ibrahimu Chabanya aliibuka mfungaji bora, John Beko kipa bora huku Victor Isack akiibuka mchezaji bora na hivyo wote watatu kujinyakulia kiasi cha shilingi elfu kumi kila mmoja (10,000).

Mwandaaji wa michuano hiyo Hilane Mwanzalima alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji katika wilayani Sengerema ambapo aliahidi kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu.

"Lengo ni kuibua na kuendeleza vipaji hasa kwa vijana wa wilaya ya Sengerema pamoja na kuwaweka watu pamoja".Alisema Mwanzalima.

No comments:

Powered by Blogger.