LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAMSHINIKIZA NA KUMCHANGIA FEDHA ZA FOMU KAJUNA ILI AGOMBEA UDIWANI KATA YA MBUGANI JIJINI MWANZA.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja Jijini Mwanza (Chadema) Richard Daniel Kajuna akizungumza jana katika kikao maalumu na baadhi ya wawakilishi wa Makundi mbalimbali ambayo yamemwomba agombee Udiwani katika Kata ya Mbugani ambapo makundi hayo yalimchangia fedha kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea.
 Na:George GB Pazzo
Makundi mbalimbali kutoka Kata ya Mbugani Jijini Mwanza yamejitokeza na kumshinikiza Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja uliopo Katani humo (Chadema) Richard Daniel Kajuna ili agombee nafasi ya Udiwani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba 25 mwaka huu.

Makundi hayo ambayo yanatoka katika Kata hiyo ni pamoja na Wajasiriamali, Waendesha pikipiki (bodaboda), Wanaharakati wa Masuala ya Siasa na Kijamii, taasisi ya Michezo na Usafi wa Mazingira DHULU Sports Club pamoja na Kikundi cha kusaidiana cha Vijana Unguja UVIMA.

“Kutokana na Umoja wetu wa kufanya shughuli za Kijamii tuliamua kwa pamoja kumuomba Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja kwamba ni Vyema akagombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mbugani, na hii ni kutokana na harakati zake za kimaendeleo alizonazo na tunaamini kwamba tukishirikiana nae tutafanikisha maendeleo miongoni mwetu”. Alisema mwakilishi wa Makundi hayo wakati wa kikao kifupi cha kumuomba na kumchangia Kajuna fedha kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea kilichofanyika jana katika Shule ya Msingi Mbugani.

Katika kikao hicho, jumla ya Shilingi Elfu Hamsini na tano (sh.55,000) zilipatikana na hivyo kufanikiwa kufikisha gharama za kumwezesha Kajuna kuchukua fomu ya kugombea Udiwani ambapo gharama ya kuchukua fomu hiyo ni shilingi Elfu Hamsini (Sh.50,000).

Mwenyekiti huyo wa Mtaa wa Unguja Jijini Mwanza (Chadema) Richard Daniel Kajuna alikubali kulipokea ombi hilo ambapo alieleza kuwa yuko tayari kugombea udiwani katika Kata hiyo ya Mbugani mwaka huu kupitia Ukawa kadri ratiba itakavyotolewa na viongozi wake wa ngazi za juu.

“Nitakapokuwa diwani ingawa watu wanasema nitauliwa na mahasimu wangu wa kisiasa hilo naomba niliweke wazi, nitaanza na kutetea shule ya Msingi irudi kwa wananchi, nitajali vikundi mbalimbali kwa fedha zinazotoka halmashauri ya jiji la Mwanza ili fungu linalotoka liwanufaishe wahusika na nitaweza pia kusimamia vyema miradi mbalimbali katika Kata yangu ukiwemo mradi wa Majitaka ambao uko katika Mtaa wa Unguja”.Alisema Kajuna.


Baada ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mwaka 1995, Kajuna aliwahi kuwa Katibu wa Chama hicho Tarafa ya Inchugu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara tangu mwaka huo hadi mwaka 2000 ambapo kuanzia mwaka 2000 pia alikuwa Katibu wa Chadema Kata ya Mirongo hadi mwaka 2010 kabla ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja uliopo Kata ya Mbugani zote Jijini Mwanza.

Wakati Makundi hayo yakijitokeza kumshinikiza Kajuna kugombea Udiwani, tayari aliekuwa diwani wa Kata ya Mbugani (Chadema) Hassan Kijuu ameeleza nia yake ya kutetea kiti chake baada ya kubainisha kwamba ameombwa kufanya hivyo na wananchi wa Kata hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja Jijini Mwanza (Chadema) Richard Daniel Kajuna
Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja Jijini Mwanza (Chadema) Richard Daniel Kajuna akizungumza baada ya kuombwa agombee udiwani katika Kata ya Mbugani Jijini Mwanza katika uchaguzi wa Mwaka huu 2015.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja Jijini Mwanza (Chadema) Richard Daniel Kajuna akizungumza jana katika kikao maalumu cha Kumuomba rasmi agombee Udiwani katika Kata ya Mbugani pamoja na kumchangishia fedha kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ambapo jumla ya Shilingi Elfu Hamsini na tano zilipatikana na hivyo kufikisha gharama za kuchukua fomu ambazo ni shilingi Elfu Hamsini.

Baada ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mwaka 1995, Kajuna aliwahi kuwa Katibu wa Chama hicho Tarafa ya Inchugu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara tangu mwaka huo hadi mwaka 2000. Kuanzia mwaka huo wa 2000 pia alikuwa Katibu wa Chadema Kata ya Mirongo hadi mwaka 2010. 

No comments:

Powered by Blogger.