LIVE STREAM ADS

Header Ads

UTEUZI WA DK.MAGUFULI KUGOMBEA URAIS CCM WAFUTA DHANA YA CHAMA KUGAWANYIKA.

Dr.Magufuli
Na:George GB Pazzo
Hatimae Chama cha Mapinduzi Kimemchagua Dk.John Pombe Magufuli kuwa Mgombea wa Urais katika Uchaguzi wa Mwaka huu unaotarajiwa kufanyika octoba 25 mwaka huu 

Wadadisi wa kisiasa wanasema kuwa maamuzi hayo yamefuta hofu iliyokuwa imeanza kujitokeza ya kwamba CCM itagawanyika baada ya majina ya baadhi ya watangaza nia walioonekana kuwa na ushawishi mkubwa hususani kwa wananchi kuenguliwa mapema.

"Uteuzi wa Dk.Magufuli umepokelewa vyema na wanaccm pamoja na wajumbe tulio wengi kutoka ndani ya Mkutano Mkuu hivyo ile dhana iliyokuwa inadhaniwa kuwa ingejitokeza kuwa huenda CCM itaparanganyika imeonekana kufutika kwani hatuna hofu na utendaji wake".Alisema mmoja wa makada wa CCM hapa nchini.

Katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli alichaguliwa kwa kura 2104 sawa na asilimia 87.01, akifuatiwa na Balozi Amina Salum Ali aliyepata kura 253 sawa na asilimia 10.4 ambapo Asha Rose Migiro alipata kura 59 sawa na asilimia 2.44702.

Akitangaza Matokeo hayo hii leo majira ya saba mchana, Msimamizi mkuu wa uhesabuji wa Kura Anne Makinda alisema kuwa jumla ya kura zilizopigwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kumchagua Mgombea urais ndani ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu ni kura 2422 ambapo kura zilizoharibika ni sita na kura halali zikiwa ni 2416.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mgombea Urais ndani ya CCM, Dk.Magufuli alimtangaza mwana mama aliejizoelea umaarufu mkubwa katika bunge maalumu la Katiba Samia Suluhu Hassa ambae ndie aliekuwa Makamu Mwenyekiti katika bunge hilo kuwa mgombea mwenza wake wa urais na hivyo kuingia katika historia ya mgombea mwenza wa kwanza upande wa akina mama katika nafasi hiyo.

Upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, CCM imemchagua Dk.Ali Mohamed Shein kwa Mara nyingine kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho.

No comments:

Powered by Blogger.