LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: "UMUHIMU WA KUFUATA NDOTO YAKO" SEHEMU YA PILI.

Soama HAPA Sehemu ya Kwanza Ili Twende Sawa.
Napolion Hill aliwahi kusema chochote kile ambacho akili inachoweza kukipokea na kukiamini, akili inaweza ikakipata, jua unao uwezo sana wa kupata na kuisimamia ndoto ambayo unayo katika maisha yako.
Baada ya mtu kupata ndoto fulani kuna maswali makuu mawili ambayo mtu anatakiwa kujiuliza ambayo ni haya yafuatayo...
Swali la kwanza ni; je nipo tayari kutendea kazi hii njozi yangu? Hili ni swali la msingi sana pindi unapopata njozi fulani ambayo unataka kuitimiliza, uzuri ni kwamba kila ndoto unayoipata unayo uwezo mkubwa wa kuitimiliza hata kama ipo kinyume na kile ulichojifunza, ni suala la kujifunza namna tuu ya kukitimiliza.
Kuwa tayari maana yake ni kujitoa na kufanya jambo lolote lile ambalo utatakiwa kulifanya ili kutimiliza ndoto yako..kama ni kuondoka sehemu uliyopo kwenda sehemu nyingine itakubidi utoke na uende hiyo sehemu.... Siku za karibuni nimekuwa nikisoma kitabu cha Eric Shigongo How I move from poverty to success,wakati Shigongo kapata ndoto ya kuanzisha kampuni yake ya kuchapisha magazeti Leo hii inajulikana kama Global Publishers ilimbidi kusafiri kwenda Dar-es-salaam ili atimize ndoto yake maana kwa kipindi kile vitu ambavyo vingempelekea kutimiza hiyo ndoto yake vilikuwa vinapatikana Dar.
Vivyo hivyo kama inabidi urudi shuleni ili usome kitu fulani ambacho kitakupelekea kutimiliza ndoto yako basi uwe tayari kurudi shule, kama ni watu fulani muhimu unatakiwa kukutana nao basi unafanya jitihada zote kukutana na hao watu.
Kuwa tayari inamaanisha kutokuogopa kutenda yote yatakayopelekea kupata njozi yako, watu wengi wanakufa na ndoto zao kwa sababu ni waoga hutakiwi kuogopa maadamu tayari una ndoto unayotaka kutimiliza kwa wewe kuwa mwoga ni kufunga milango ya ndoto yako kutimia.
Kuwa tayari ni kutokusikiliza mtu yeyote yule ambaye anakuambia ile ndoto yako ambayo unataka kuitimiliza haiwezekani, inamaanisha kusikiliza moyo wako kutenda kile ambacho kinatoka ndani ya kilindi cha moyo wako kwa kujitoa kwa hali ya juu, mtu alie tayari kufanya jambo fulani hasikilizi watu wanasema nini anamanya maadamu ni kitu anchokipenda na ni kitu sahihi kwake kufanya.
Mwanamziki ambaye alikuwa maarufu sana ulimwenguni miaka ya 1990's 2pac Shakur aliwahinkusema hasara kubwa katika maisha siyo kufa bali ni kufa pasipo kutendea kazi ndoto yako. Alikuwa sahihi sana na hii ni kweli kabisa watu wengi wanakufa na ndoto zao leo hii katika nchi yetu ya Tanzania tungekuwa na kina Edison wengi lakini watu hawasimamii kile ambacho mioyo yao inawaambia watende.
Kitu kingine cha msingi hapa ni kwamba usiangalie au isiogope kutenda ndoto yako kisa unaona itakuchukua muda kuitimiza, maana pindi utakavyoitimiza utajisikia vizuri sana, utajiona mtu mwenye nguvu na anaeweza kutenda jambo lolote ambalo moyo wako unataka kwa nguvu na kwa ufasaha.
Lakini pia wewe ambaye unaeacha kufanyia kazi ndoto yako kisa ni muda ambao unaona itachukua ushawahi kujiuliza kama hata kama usipoifanyia kazi kama muda hautaenda? jibu ni rahisi muda utaenda tuu ufanyie kazi au usifanyie kazi hivyo hakuna sababu ya kuacha kuitendea kazi njozi yako kisa ni muda ambao itakugharimu.
Swali la pili ni je ninaweza kutendea kazi ndoto yangu?
Watu wengi huwa wanakata tamaa mapema sana baada ya kupata ndoto fulani alafu wakagundua hawana sifa za kutimiliza ndoto ile basi huwa wanaachana na ndoto zao. Lakini nataka nikupe moyo kwamba unao uwezo mkubwa kabisa wa kutimiza ndoto yako hata kama wewe ni mwanahistoria na una ndoto ya kutengeneza kompyuta maadamu tuu upo tayari kujifunza na kufuata hatua zote.
Nimalizie kwa mfano huu Sir Edmund Hillary na msaidizi wake Tenzing Norgey walikuwa na ndoto ya kupanda mlima Evarest, kipindi kile kulikuwa na historia,sababu na ushahidi wa kutosha wa watu ambao walipanda mlima Everest na kufa na wengine walirudia njiani na kusema haiwezekani. Lakini hawa watu wawili hawakukata tamaa wala kusikiliza maneno ya watu bali waliendelea kushikilia ndoto yao ya kutaka kupanda mlima Everest na wawe juu ya kilele cha dunia. Mwaka 1951 wakapanda mlimani lakini walirudia njiani watu wakawa wanawaambia wamshukuru Mungu maana wamerudi salama ila wao waliendelea kushikilia ndoto yao na hawakutaka kabisa kukata tamaa walikuwa tayari kufanya chochote kile ili kutimiliza ndoto
Mwaka 1952 wakapanda tena mlima Everest wakashindwa sasa kumbuka walikuwa wanatumia fedha, walikuwa wanatumia na muda wao na ilikuwa ni hatari kwa kipindi kile maana hakuna mtu yeyote aliewahi kufika kilele cha Mlima Everest watu wakaanza kuwaita vichaa maana walikuwa wanaenda mara kadhaa na kurudi pasipo mafanikio ya aina yoyote ile.
Ilipofika mwaka 1953 wakajipanga tena kwa mara nyingine wakaenda na ndio mwaka waliofanikiwa na kuwa watu wa kwanza kufika kwenye kilele cha mlima mrefu zaidi kupita yote duniani. Je kama wangeamua kuachana na ndoto yao kwa kusikiliza watu wangeweza? Na je kama sio wao kuthibitisha kwamba inawezekana kupanda mlima Everest kuna mtu angekaa apande? Ni mamilioni ya watu wamekuwa wakipanda mlima Everest baada ya wao kuthibitisha kwamba inawezekana. Hebu na wewe sibitishia ulimwengu kwamba unaweza kutimiza hiyo ndoto yako ambayo unayo kwa kuitendea kazi mpaka ilete matunda. Kitu ambacho watu wengi hawafahamu na mimi ngoja nikufahamishe leo ni kwamba Edmund Hillary alikuwa mfuga nyuki kutokea Newzeland sasa wewe unaogopa nini kuhakikisha unatimiliza ndoto yako?
Ndio unaweza...kutimiza ndoto uliokuwa nayo kama ukiamua kuchukua hatua zote muhimu na kujitoa kwa dhati katika hicho ambacho unakiamini.
Itaendelea sehemu ya Tatu..
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY YA JIJINI MWANZA AMBAO NI WATAALAMU WA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI.
Email:allnhumph@gmail.com Phone: 0689 45 26 70/0765 53 68 42

No comments:

Powered by Blogger.