VIDEO MPYA YA "SIHA TOTOZINA" IITWAYO "YA LEO SIYO YA JANA" NI BURUDANI TOSHA.
Mwanamuziki SIHA TOTOZINA kutoka Mkoani Mwanza
Mwanamuziki Siha Totozina kutoka Mkoani Mwanza ameachia Video ya Wimbo wake uitwao YA LEO SIYO jana ambapo Video hiyo imetengenezwa na Producer Michael kutoka King Mega Video huku audio ikitengenezwa na Producer Simba Mkali kutoka Masai Music."Hii ni Video yangu ya Kwanza hivyo naomba mashabiki wangu waipokee vyema na ujumbe ambao nimejaribu kuufikisha humo ndani ni juu ya kipaji changu cha uimbaji nikiiambia jamii kwamba Muziki ni kazi kama kazi nyingine hivyo wasinidharau mimi kuwa mwanamuziki, na kwamba majungu wanayonipa ipo siku nitawin (nitashinda) na watanithamini. Totozina ameiambia Binagi Tv ya Binagi Media Group.
Video hii ina changamoto zake kuanzia kwenye AUDIO hadi katika VIDEO, Binagi Media Group tunaifikisha kwako itazame na kusikiliza vyema kile ambacho Msanii pamoja na Producers wote (Audio na Video) walichokifanya kisha toa ushauri wako kupitia nambari 0753 166 323.
Bonyeza Play hapo chini Kuitazama Video hiyo ya Siha Totozina-Ya Leo Siyo Ya Jana.
Mwanamuziki SIHA TOTOZINA kutoka Mkoani Mwanza
No comments: