LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAADA YA MHE.SUMAYE KUZUSHIWA KUHAMIA CHADEMA, UKWELI WABAINIKA.

Na:Judith Ferdinand
Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Frederick Sumaye,juzi amezushiwa kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kuchoshwa na demokrasia uchwara na kutoridhishwa na mchujo wa wagombea ndani Chama cha Mapinduzi CCM.

Akizungumzia uvumi huo jana, aliyekuwa Meneja Kampeni wa Sumaye wakati wa mchakato huo wa urais John Lema, amekanusha taarifa hizo za mitandao kuwa, ni za uzushi na uzandiki zilizolenga kumchafua.

Alisema hadi sasa Waziri Mkuu mstaafu huyo bado ni mwana CCM, hafikirii kuhamia chama chochote cha upinzani kama ilivyovumishwa na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Alisema kuwa Sumaye ambaye alikuwa miongoni mwa watangazania 42 wa CCM, alikubaliana na matokeo ya mchakato huo baada ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kubuika mshindi na aliahidi kumwunga mkono kwa kuzunguka nchi nzima kumfanyia kampeni ya kusaka kura.

Lema alisema baadhi ya mitandao ya kijamii,ilikuwa na taarifa za kwamba Sumaye aliitisha mkutano wa Waandishi wa habari, uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, akawaeleza kuwa amejiunga na Chadema, moja ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)

“Juzi, mtandao mmoja katika habari za hapo hapo(Breaking News), uliandika kuwa, Waziri Mkuu mstaafu,kuongea na waandishi wa habari Idara ya habari Maelezo,atatoa ya moyoni,kuhusu mchakato wa kumpata mgombea Urais na ataweka wazi mstakabali wake wa kisiasa.”

“Mtandao mwingine, wenyewe uliandika kuwa, Waziri Mkuu wa zamani,amejitoa CCM na kujiunga na Chadema/Ukawa,amezungumza na wanahabari Court Yard  hoteli,akidai amechoshwa na demokrasia uchwara ndani ya CCM”. Alisema Lema alinukuu mitandao hiyo ya kijamii ambayo hakuitaja.

Alisema habari hizo hazina ukweli, kwani hivi sasa Sumaye hayupo Dar es salaam, yuko kijijini kwake akimwuguza mama yake mzazi, na ameshangazwa na uvumi huo usio na kichwa wala miguu wa kumhusisha na kuhamia Ukawa kwa sababu hajawahi kufikiria kuhama ndani ya CCM kwa kukosa nafasi ya kuchaguliwa.

“Nimezungumza na mzee Sumaye,ahabari hiyo imemletea usumbufu ndani ya familia,marafiki,Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu na CCM yenyewe.”

“Kwa hiyo anawahakikishia watanzania wana CCM kuwa, bado ni mwanachama mtiifu na mwaminifu,hana fikra za kuhama.Yaliyotokea Dodoma yaliyofanywa kwa kufuata kanuni na taratibu za CCM  ili kumpata mgombea urais wa chama chetu”. Alisema Lema na kuongeza;

“Binafsi Sumaye anamwunga mkono mteule wa CCM wa Urais (John Magufuli) na atazunguka nchi nzima kumfanyia kampeni mgombea huyo kwa kumwombea kura ili kuhakikisha anashinda ili CCM iendelee kushika dola”.


Katika hatua nyingine Lema alimpongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa kusaini sheria ya mtandao ambayo alisema kuwa itakapoanza kutumika itakuwa mwarobaini wa watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.

No comments:

Powered by Blogger.