LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MSASA JUU YA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU.

KUMEKUEPO NA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU HUSUSANI WATOTO KUTOKA NCHI ZA KIAFRIKA KWENDA NCHI ZA UGHAIBUNI KWA AJILI YA KWENDA KUTUMIKISWA KIKAZI.

Nchini Tanzania juzi Wanahabari walipewa Semina juu ya Biashara hiyo haramu ili waweze kusaidia kuitokomeza!
Unadhani nini kinasababisha biashara hiyo inashabiri Barani Afrika?
Afisa Mwandamizikutoka Sekretarieti ya kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Alex Lupiya akitoa mada wakati wa semina kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi juzi Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora, Joshua Taramo akitoa mada wakati wa semina kwa waandishi wa vyombo vyaha bari Nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,juzi Jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa kituo cha Televisheni Azam, Ismail Hamza, akiuliza maswali wakati wa semina kwa waandishi wa vyombo vya habari Nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,juzi Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Nchini wakimsikiliza Msaidizi wa mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, John Makuli(hayupopichani), wakati akiwasilisha mada kwenye semina kwa waandishi wa vyombo vya habari Nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, juzi Jijini Dar esSalaam.
PICHA ZOTE NA ABUBAKARI AKIDA,WIZARAYA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Powered by Blogger.